KURASINI SDA KWAYA WAPATA VYOMBO VIPYA VYA MUZIKI
mwambawahabariblog
Na John Luhende
mwambawahabariblog
mwambawahabariblog
Katika
kuhakikisha Injili ya Yesu kristo ina
hubiriwa kwa mataifa yote watu watatu ambao majina yao tumeya hifadhi wameonekana kuwa ni wenye mapenzi mema na kazi
ya Mungu wamejitolea kununua
vyombo vya muziki PA SYSTEM katika kanisa la
Waadventista Wasabato kurasini ambapo vyombo hivyo vina thamani ya shilingi milion saba na laki tatu ,vitatumika na kwaya ya kanisa hilo ambayo ina julikana
kama Kurasini SDA Kwaya , au kwajina la
utani (Fuso).
Akiendesha
huduma ya kuweka waqifu vyombo hivyo mzee wa kanisahilo Joseph Nganga , amewaomba wasamaria wengine kuguswa na kazi ya
Mungu na kuendelea kuchangia kwakuwa bado kuna upungufu wa vyombo vya muziki nakuwataka kutambua uthamani wa
kwaya hiiyo,akitoa mfano wa kujulikana kwa kwaya hiyo mzee Nganga alisema
“ majuma
machache yaliyopita mama mmoja kutoka
mwanza alikuwa akitafuta kanisa lakwaya
hiyo lilipo iliaje
kusikiliza nyimbo na kuchangia fedha kwaajili
ya huduma kwa kazi ya Mungu, alipata taabu sana kuwakuwa alikuwa hapafahamu
mahali lilipo kanisa , alipotea lakini
mwishowe alifika , hii inaonyesha ni namna gani kazi hii ya waimbaji ilivyo wafikia watu wengi
haijalishi wako umbali kiasi gani “ alisema mzee nganga.
Katika hatua
nyingine kanisa hilo kufuata utaratibu
wa kanisa la Wasabato ulimwenguni washiriki wa kanisa la Wasabato kurasini wameingia katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kugawa
vitabu 270 vikiwemo vya TUMAINI KUU pamoja na vitabu
vya SABATO YA KWELI na badhi ya
vipeperushi (vijizuu) ilikupeleka injili
kwa watu wote wamfahamu Kristo waache dhambi wamchemungu waokolewe .
Post a Comment