WAHANDISI TEMESA WATUNUKIWA VYETI
mwambawahabariblog
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase OleKujan ( wa sita kulia waliosimama) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa Mafunzo ya teknolojia ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology) kutoka TEMESA.
Na Theresia Mwami
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi
Manase Ole Kujan, wamewatunuku baadhi ya waandisi na mafundi wakati akifunga
mafunzo ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology) kwa watumishi wa
TEMESA.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wiki mbili, yametolewa kwa
kushirikia na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Fizikia, kwa watumishi
20 wa TEMESA kupata mafunzo ya nadharia na vitendo.
Katika hotuba yake Mhandisi Manase aliushukuru uongozi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuendesha mafunzo hayo kwa wataalamu wa
TEMESA, kwani yatawapa uwezo wahandisi na mafundi wa kuendana na mabadiliko ya
sayansi na tekenolojia.
“Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana
katika maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya
wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika
kuandaa na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme
nchini.” Alisema Mhandisi Manase.
Aidha, TEMESA inasimamia miradi mbali mbali ya teknolojia ya umeme
wa jua nchini ikiwemo mfumo wa teknolojia ya umeme wa jua kwa shirika la
utangazaji Tanzania (TBC) Songea, mfumo wa teknolojia ya umeme wa jua katika
ofisi ya Rais Utumishi, kusimamia na kuhakiki mifumo ya teknolojia
ya umeme wa jua inayofungwa vijijini katika mikoa ya Geita, Kigoma Ruvuma
na Tabora iliyo chini ya REA, kusimamia matengenezo ya mifumo ya teknolojia ya
umeme wa jua katika ofisi zote za TRA pamoja na miradi mbali mbali ya taa za
kuongozea magari barabarani zinazotumia teknolojia ya umeme wa jua.
Post a Comment