HOSPITAL YA TAIFA MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI WA PUA, MASIKIO
Katika chumba namba moja, madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakifanya upasuaji wa pua kwa mgonjwa LEO kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hispania. Kutoka kushoto ni Martin Mushi, Pedro na Carlos wakifanya upasuaji kwa mgonjwa mwenye matatizo katika mfumo wa pua.
Chumba namba mbili, madaktari wakifanya upasuaji wa masikio kwa mgonjwa mwenye tatizo masikio LEO.
Madaktari wakiendelea na upasuaji wa masikio LEO katika chumba namba mbili.
Madaktari wakifanya maandalizi kabla ya kufanya upasuaji LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
………………………………………………………………………………………..
Neema Mwangomo, PRO MNH
Dar es Salaam, Tanzania. Madaktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na timu ya Madaktari wanne kutoka nchini Hispania waaendesha zoezi la upasuaji wa masikio , pua pamoja upasuaji wa shingo na kichwa (Head and Neck Surgery).
Akizungumzia kuhusu zoezi hilo Daktari Bingwa wa magonjwa ya masikio, Pua na koo Martin Mushi amesema katika upasuaji huo madaktari hao wanatumia teknolojia kubwa na ya kisasa zaidi ambapo pamoja mambo mengine ujio wao utawawezesha madaktari wa Muhimbili kujifunza zaidi matumizi ya teknolojia mpya ya upasuaji (ENDOSCOPY SURGERY).
Akifafanua Daktari Mushi amesema awali wagonjwa hao walikuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji, lakini kwa sasa wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa kawaida wanapata huduma hiyo hopa Muhimbili.
Kwa mujibu wa Daktari Mushi, tangu zoezi hilo lianze jumatatu ya wiki hii mpaka sasa wagonjwa 16 tayari wamefanyiwa upasuaji na kwamba hadi kukamilika kwa zoezi hilo wagonjwa kati ya 25 hadi 30 watakuwa wamefanyiwa upasuaji huo.
“Zoezi hili linaendelea vizuri tunashirikiana vema na wataalamu hawa kutoka nchini Hispania, ni fursa nzuri kwakweli kwani tunabadilishana uzoefu, lakini kubwa zaidi sisi kujifunza kutoka kwao,” amesema Dk Mushi.
Zoezi la upasuaji kwa ushirikiano na timu ya watalaamu kutoka Hispania limeanza Aprili 18 , 2016 na linatarajia kumalizika April 22, 2016.
Post a Comment