ICHAWA yazindua mfumo shirikishi kwa bodaboda
Na Beatrice Lyimo
mwambawahabariblog
Uongozi wa kampuni ya Kikundi cha
Waadhirika wa Maendeleo (KICHAWA) unaojishughulisha na usafirishaji wa mizigo
wamezindua mwongozo wa mfumo shirikishi wa uratibu wa Bodaboda na
Bajaji nchini.
Akizindua mfumo huo leo Jijini Dar
es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Mussa Chengulla na kusema kuwa
lengo ni kupambana na kupata suluhiso la kudumu katika sekta ya usafirishaji wa
Bodaboda na Bajaji juu ya changamoto za kisheria, kiusalama na kimazingira.
Chengulla amesema kuwa sababu
zilizopelekea kuanzishwa kwa mfumo huo ni matokeo makubwa ya changamoto
zilizojitokeza katika jamii juu ya wizi wa pikipiki, wizi wa kutumia pikipiki,
uvunjifu wa sheria za usalama barabarani, kanuni za usafirishaji, matumizi ya
kujichukulia sheria mkononi, uegeshaji holela wa bodaboda na bajaji na
ukamataji usio salama.
“Uwanzishwaji wa mfumo huu
shirikishi ni kukabiliana na changamoto zitokanazo katika sekta ya usafirishaji
na kutatua kero hatarishi zinazoikabili jamii ili kufika malengo ya kuiondoa
ajira ya bodaboda na bajaji katika orodha ya ajira hatarishi, kero na janga la
Taifa na kuifanya kuwa ajira tegemezi, endelevu na salama kwa usalama wa raia
na mali zao” aliongeza Bw. Chengulla.
Mbali na hayo Bw. Chengulla amesema
kuwa watakaonufaika na mfumo shirikishi ni TAMISEMI Halmashauri ya Manispaa ya
Wilaya kwa kutambua idadi kamili ya wanaoendelea kujiajiri na kuajiriwa kupitia
sekta ya usafirishaji abiria.
Pia wengine watakaonufaika na mfumo
huo shirikishi ni SUMATRA, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Jeshi la Polisi na
Usalama ya Raia na kitengo cha usalama barabarani, wamiliki na madereva wa
bodaboda na bajaji kulingana na kazi za sekta husika.
![]() |
Click here to Reply, Reply
to all or Forward
|
Post a Comment