Ads

MultiChoice Africa yatangaza HAKUNA ONGEZEKO LA BEI kwa Wateja Wa DStv.

 

Umekuwa mwaka mgumu kwa MultiChoice Africa. Masoko yetu yameathirika kutokana na kuporomoka kwa bei ya bidhaa na mafuta na kushuka kwa thamani ya shilingi ya kitanzania. Gharama nyingi za MultiChoice zipo katika dola ya Kimarekani kitu ambacho kilitulazimisha kuongeza bei katika mwaka 2015.

Lakini hatupo peke yetu, wateja wetu ambao ni rasilimali yetu kuu, wanateseka. Kwa hiyo tutafanya kitu kidogo. Tumeamua kujitwisha sehemu ya mateso na hivyo HATUTAONGEZA bei kwa wateja wa vifurushi vyote vya DStv kama ambavyo tumekuwa tukifanya kila mwezi Aprili. Pasipo majanga mengine ya kiuchumi yasiyotarajiwa, hatutarajii ongezeko la bei katika mwaka huu wa 2016.  


Wateja ndio sababu ya uwepo wetu, kwa hiyo tunadhamiria kuwaletea maudhui na vipindi bora kabisa kwa bei nafuu. Tunataka muwe na wakati na uzoefu murua wa burudani za hapa nyumbani na kimataifa katika televisheni.

Tuliianza safari mwezi uliopita tulipozindua chaneli mpya za SuperSport ili kuwaletea Ligi Kuu Ya Uingereza (EPL), Ligi Kuu ya Hispania(La Liga) na Michuano Ya Mataifa Ya Ulaya (EURO 2016) kwa wateja wa kifurushi cha DStv Compact na hatuishii hapo. Mwezi huu wa Aprili, chaneli za DStv zitaonyesha misimu mipya na kisasa kabisa ya vipindi mfululizo ukiwemo msimu wa 6 unaosubiriwa kwa hamu wa Game Of Thrones kuanzia kwenye M-Net Edge, Express kutoka US, sambamba na telenovela mpya ya Hush ndani ya Africa Magic Showcase na The Voice: Nigeria. Wateja pia wataburudishwa na chaguo za shoo mbalimbali za burudani za ndani na kimataifa zinazopatikana katika vifurushi vya DStv ikiwemo telenovela mpya ndani ya Zee World, East Meets West wakati marathoni ya maudhui ya filamu “Wedding Season” ndani ya chaneli ya Universal itakonga mioyo ya watazamaji kwa chaguzi kabambe za filamu za mapenzi na vichekesho. Marathoni zaidi zinawasubiri ndani ya Studio Universal ambapo ‘Manscape’, ‘April Fools’, ‘Getting Away With it’ na marathoni za Steven Spielberg zitawaacha na vicheko na msisimko.

Waigizaji wa Hollywood wenye mvuto na wanaong’ara zaidi wataonyeshwa kupitia E! Entertainment huku #Richkids Of Beverly Hills ikirudi na onyesho la kwanza la LA Clippers Dance Squad. Jipatie kiti cha mbele kushuhudia nyota maarufu wanapopita katika zulia jekundu katika maonyesho yaliyosheheni nyota wa uigizaji na burudani katika Black Girls Rock 2016 ndani ya BET na 2016 MTV Movie Awards ndani ya MTV Base. Mashabiki wa soka na wateja wa vifurushi vya DStv Premium, Compact Plus na Compact pia watapatiwa burudani ya maonyesho ya moja kwa moja kutoka mechi za  Ligi Kuu Ya Uingereza (EPL), Ligi Kuu Ya Hispania (La Liga) na michuano ya Kombe La Mataifa ya Ulaya 2016(Euro 2016) ndani ya SS3, SS11 na SS12 huku upande wa Hispania wakijiandaa na mechi inayosubiriwa kwa hamu ya El Classico kati ya Barcelona na Real Madrid tarehe 3 Aprili.

Kaimu Meneja Mkuu, Francis Senguji amesema, “ Tunayo furaha kubwa kutangaza kwamba hakutokuwa na ongezeko la bei katika vifurushi vyote vya DStv Aprili hii. Pasipo majanga mengine ya kiuchumi yasiyotarajiwa, hatutarajii ongezeko la bei katika mwaka huu wa 2016.  Kwa maana hiyo mwezi ujao, wateja wa DStv watarajie kuendelea kupata burudani za kuvutia kutoka DStv pasipo gharama zozote za ziada”

Kwa taarifa zaidi juu ya vifurushi na vipindi au shoo zijazo, tafadhali tembelea www.dstv.com

Image result for nembo ya multichoice africa

No comments