WAZIRI MUHONGO AITAKA KAMPUNI YA TANZU YA TANESCO (TGDC) KUHARAKISHA UZALISHAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI KUTOKA ZIWA NGOZI
mwambawahabariblog
Waziri wa Nishati na Madini,
Prof. Sospeter Muhongo ameiaigiza Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi
Tanzania (TGDC Ltd) kuwa ifikapo June 2016, iwe imeanza kuchoronga mashimo 3
katika eneo la Ziwa
Ngozi ikiwa ni hatua ya mwisho inayohitajika kabla ya
kuanza kujenga mitambo ya kuzalisha jotoardhi.
“Utafiti
muhimu umekamilika. Joto la maji ni kubwa, 230-250C linalokidhi uzalishaji wa
umeme. Hiki kitakuwa ni chanzo kipya muhimu cha umeme jadidifu”
,alisema Prof. Muhongo.
,alisema Prof. Muhongo.
Ameongeza
kuwa, jambo hilo haliwezi kuendelea kusubiri kutokana na mahitaji ya nishati
hiyo nchini ikizingatiwa kuwa, Tanzania inapitiwa na Bonde la Ufa kwa
kiasi kikubwa.
“Tayari
wenzetu Kenya na Ethiopia wamepiga hatua kubwa katika nishati hii lakni kwa
upande wetu hatuna megawati hata moja kwa hili lazima tuchukue hatua tutoke
hapa tulipo. Hakuna kusubiri anzeni na Ziwa Ngozi” amesema Muhongo.
Prof.
Muhongo aliitaka Kampuni hiyo kuongeza nguvu katika eneo lenye viashiria vya
jotoardhi la Ziwa Ngozi kutokana na kuwepo maendeleo makubwa ya kitafiti
ikilinganishwa na maeneo mengine yenye viashiria kama hivyo ikiwemo eneo la
Mbaka lililopo Wilaya ya Rungwe.
“TGDC
tunataka umeme wa jotoardhi, wananchi wanataka umeme, hawatakuwa kusikia
maneno, ifikapo Mwezi juni na mimi nitakwenda Ngozi kuangalia mmefikia
wapi na kama hakuna maendeleo tutabadilisha timu ya wataalamu”, alisisitiza
Prof. Muhongo.
Akizungumzia
kuhusu fedha za miradi, Prof. Muhongo alieleza kuwa, nchi nyingi duniani
hazitegemei fedha za Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya nishati na
ndiyo sababu hata Tanzania inatafuta fedha katika taasisi mbalimbali ikiwemo
kukaribisha wawekezaji ili kutekeleza miradi hiyo.
“Serikali
kwa upande wake itasaidia kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi
na ninyi kazi yenu ni kuhakikisha umeme wa jotoardhi unaanza kutumika Tanzania
kwa kuanza na Ziwa Ngozi”.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa amefarijika na maelekezo
aliyoyatoa Prof. Muhongo na kuahidi kuweka nguvu kubwa katika kufuatilia suala
hilo. ” Ujio wako umetupa ari mpya katika kusimamia miradi hii kwa sababu
rasilimali zipo lakini zimekaa tu nakuahidi kasi ya ufuatiliaji itaongezwa”,alisema
Kandoro
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rugwe ,Mwalimu Zainabu Mbusi alieleza kuwa
maagizo ya Prof. Muhongo yamekuwa faraja na kuongeza kuwa, kukamilika kwa mradi
huo itaongeza kasi ya ukuaji uchumi na kuifanya Tanzania kufikia lengo lake la
kuwa miongoni mwa nchi za uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Kwa
pande wake Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Fred Atupele alieleza kuwa,
kukamilika kwa mradi huo kutachochea kasi ya uendelezaji wa viwanda vikubwa na
vidogo na kueleza kuwa, kwa nafasi yake watachukua jukumu la kuwaelimisha
wananchi kuhusu umuhimu wa vyanzo hivyo.
Awali
akieleza akieleza Mikakati ya Taasisi hiyo, Mkurugenzi wa TGDC , Mhandisi
Boniface Njombe alisema eneo la Mbaka ni miongoni mwa maeneo ya maji moto yenye
viashiria vya nishati ya jotoardhi.
Vilevile,
alieleza hivi sasa wataalam kadhaa wamesambaa wakifanya tafiti za mwisho
katika eneo la Mbaka ili kuanisha mipasuko na maeneo ya kuchimba nishati
hiyo na kuongeza kuwa, TGDC imelenga kwa kuanza kuzalisha umeme wa
jotoradhi wa kiasi cha megawati 200 huku lengo ikiwa ni kufikia
megawati 5000.
Aidha,
alieleza kuwa, mbali na kuzalisha umeme , maji moto yanaweza kutumika viwandani
na majumbani katika kukausha mazao ikiwemo kuwa kivutio cha utalii kuoga kwa
kuwa inaelezwa kuwa maji hayo yanatajwa kuwa tiba ya magonjwa ya ngozi.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi zinazopitiwa na Bonde la Ufa eneo ambalo linatajwa kuwa na
viashiria vya nishati ya jotoardhi.
Post a Comment