BENKI YA WANAWAKE YATAKIWA KUWAWEZESHA KIUCHUMI NA KIELIMU WANAWAKE
mwambawahabariblog
Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu, ameitaka Bodi na Watendaji wa
Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), kuhakikisha kuwa inawawezesha wanawake
kiuchumi kwa kufikisha huduma hiyo mbali zaidi ili kuifanya benki kuwa kimbilio
la wanawake kweli .
Akizungumza katika ziara
yake ya mafunzo katika benki hiyo akifuatana na Naibu wake waziri Dakta HAMISI
KIGWANGA, Katibu mkuu na watendaji wa Wizara hiyo UMMY alisema wanawake wa
Tanzania wanajitoa sana katika kulea familia hivyo wakiwezeshwa watakuwa
wamewezesha familia, vijana na Taifa kwa ujumla.
Waziri huyo
alisema watendaji wa benki hiyo ya wanapaswa kuweka utaratibu
mzuri wa utoaji wa huduma ambazo zitaweka fikra za wanawake pale wanapotaka
kuchukua mikopo au kuweka fedha zao katika benki kufikiria kwanza benki ya TWB.
“Mimi huwa naona
uwezeshaji wa kweli wa wanawake ni kuhakikisha kuwa tunawawezesha kiuchumi na
kielimu kwasababu mwanamke atashiriki kulima kupanda lakini ikifika kuvuna tu
mazao sio yake hivyo endapo tutapata fedha zinazohusu mfuko wa wanawake
Serikalini tutaomba zipitishwe kwenye Benki ya Wanawake na tutakwenda kila
Halmashauri kuanzisha saccos za wanawake ili waweze kupata fedha za kukopeshwa
na benki ya wanawake,’’alisema Ummy.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema benki nyingi
zilizopo hapa nchini hivi sasa hazimilikiwi na Serikali hivyo, TWB inapaswa
kuhakikisha kuwa inaweka mipango yake sawa ili iweze kubaki Serikalini kwani
lengo la kuanzishwa kwa benki hiyo ni kuleta ukombozi wa kiuchumi wa wakinamama
kwani mama ni mlezi mkubwa wa familia.
Awali Mwenyekiti wa bodi
wa benki hiyo Mohamed Nyasanaamesema tangu benki hiyo inakabiliwa na
ukosefu wa umiliki wa jengo ambapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 wamelipa
kodi ya pango shilingi bilioni mbili ambapo kila mwaka hulipa shilingi milioni
500 (mia tano).
Aliongeza kwamba pamoja
na changamoto hiyo ya kodi kubwa ya pango benki hiyo imefanikiwa kukuza mtaji
wake kutoka shilingi bilioni mbili nukta nane hadi shilingi bilioni nane nukta
tano ikiwa na wanahisa 164 huku mwanahisa mkuu akiwa msajili wa hazina ambaye
anamiliki asilimi 99 ya hisa.
Amebainisha kuwa hivi
sasa inawateja elfu 56, asilimia 77 wakiwa wanawake na asilimia 23 wakiwa
wanaume na wateja wa kampuni wakiwa asilimia tatu.
Pia benki
hiyo ina matawi mawili Mkwepu na Kariakoo vituo vya huduma sita Dodoma, Mwanza,
Njombe, Ruvuma na Iringa.
Naye Mkurugenzi wa benki
hiyo Magreth Chacha ameiomba Serikali kuwasaidia kupata fedha maalum
ili waweze kukopesha wanawake wengi zaidi kwani kwa hivi sasa TWB inauwezo wa
kukusanya shilingi bilioni saba kila mwaka.
Post a Comment