Wamiliki wa majengo wahimizwa kulipa kodi
Na Skolastika Tweneshe
mwambawahabariblogsport.com
Wamiliki wa majengo
katika Halmashauri ya Ilala wamehimizwa kulipa kodi ya majengo ili kufanikisha
maendeleo ya nchi.
Hayo yamesemwa leo na
Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shaibu alipokuwa akizungumza na
waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, amesema kuwa wamiliki wa
majengo wanapaswa kulipa kodi ndani ya siku 30 tangu anapokuwa amepewa hati ta
madai.
Ameongeza kuwa hati hizi
uanza kutolewa Julai ya kila mwaka na mlipa kodi anatakiwa kuwa amelipa ifikapo
tarehe 31/10 kila mwaka ambapo baada ya mwaka mmoja mlipa kodi atatikwa kulipa
faini ya asilimia 25 kwenye kiasi cha kodi ambacho hakijalipwa.
“Kulipa kodi ni lazima
kwa maendeleo ya nchi na kodi hii hutozwa chini ya Sheria ya mamlaka
za miji (The Urban Authorities Act) namba 2 ya 1983 na marekebisho yake 2002.”.
Alisema Tabu
Aidha Tabu Shaibu
amesema wapo wafanyabiashara wakubwa ambao bado wanadaiwa kodi ya
majengo, miongoni mwao ni Air Tanzania Company Limited Tsh 14,124,081.00,
Peacok Hotel Tsh 69,960,458.00, Mohamed Entreprises Limited Tsh 6,274,233.00,
Business Printers tsh 6,561,870.00, lamada Hotel & Apartments limited Tsh
24,483,020.00 na Yusuph Mohamed Manji & Salim J Mussa Tsh 21,020,715.00.
Kodi ya majengo ni
miongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato katika Halmashauri,
hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulipa kodi.
Post a Comment