Ads

KIWANGO CHA MAUZO YA SOKO LA HISA CHAZIDI KUONGEZEKA

Na Jesca Mathew
mwambawahabariblogspot.com
KIWANGO cha Uuzwaji wa hisa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE)kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 13 .8 nakufikia shilingi trioni moja kwa kipindi cha  mwezi January Hadi desemba mwaka huu. 
 Logo mpya inayotumika katika soko la hisa la Dar-es salaam  DSE.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Meneja Mauzo na Biashara wa soko la hisa la Dar es salaam DSE Patrick Mususa amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kuwepo kwa ongezeko la hati fungani pamoja na muamko mkubwa kwa wa wawekezaji katika kununua hisa kupitia soko hilo .

‘’Ongezeko hili la ununuzi wa hisa limetokana na ongezeko la hati fungani na kuwepo kwa mwamko mkubwa kwa baadhi ya wananchi kununua hisa zilizo katika soko hilo la hisa ‘’Alisema Patrick Mususa .

Meneja Mauzo Mususa alisema kuwa kuwepo kwa ongezeko la faida katika hisa zinazouzwa na soko hilo kumeweza kuongeza manunuzi ya hisa hali inayochangiwa na mwamko wa ununuzi wa hisa .

Alisema kuwa zaidi ya wawekezaji watapatao 200000 wameweza kujiunga na soko hilo na kuorodheshwa hali inayochangiwa na taasisi hiyo kutumia mbinu za kisasa ikiwemo za mifumo ya kieletroniki pamoja na simu katika kuuza hisa zake .






No comments