SAMATTA AWA MCHEZAJI BORA AFRICA: NAPE AMPONGEZA
mwambawahabariblogspot.com
Waziri wa Habari,
Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Nnauye amempongeza mchezaji wa
mpira wa miguu wa Taifa Star Mbwana Samatta baada ya
kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka Afrika 2016 kwa wachezaji wanaocheza
soka Barani Afrika.iliyotolewa nchini Nigeria.
Nnauye ametoa kauli
hiyo wakati wa mkutano na watumishi wa Wizara wa Habari, Utamaduni , Sanaa na
Michezo leo jijini Dar es salaam.
Amesema tuzo hiyo
imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa
nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.
Nnauye amewataka
wachezaji wengine kufuata nyayo za mchezaji huyo kwa kuongeza juhudi, nidhamu
katika michezo na watambue kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni kazi kama zilivyo
kazi nyingine.
Akifafanua zaidi
Nnauye alibainisha kuwa kilichomfikisha Samatta hapo ni kujitambua
na kujituma katika ajira yake.
Samatta ameibuka
mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza ligi ya Barani
Afrika kwa kupata alama 127 dhidi ya Robert Kidiaba aliyepata alama 88 na
Baghdad Bounedjah alama 63.
Post a Comment