Ads

AZAM FC YAWASILI DAR VICHWA CHINI BAADA YA KIPIGO CHA 2- 1




TIMU ya soka ya AZAM  FC imewasili leo ikitokea visiwani Zanzibar katika michuano ya Kombe   la Mapinduzi   inayo endelea visiwani humo  ,ambapo hapo jana timuhiyo ilipokea kipigo chambwamwizi cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa mafunzo ya zanzibar



Wachezaji wa timu hiyo walionekana kuchoka wakati wakiwasil katika Bandari ya Dar es salaam   huku wakitoka  kwa kujificha wakikwepa kamera za waandishi wa habari    mwambawahabari ilifanya kazi kubwa kuweza kunasa  sura za waachezaji hao kwambali wakati wakishuka  na kuelekea kupanda Bus lao.


Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo    Hemed Mao  akizungumza na mwambawahabari    alimesema wamekubaliana na kipigo hicho kwakuwa ni sehemu ya mchezo na sasa watahakikisha wana elekeza nguvu zao katika ligikuu Tanzania bara



Naye kocha wa timu hiyo Stewart Hall   amesema wamefungwa na mafunzo kwasababu wachezaji hawa kujituma lakini wana uhakika wata fanya vizuri katika  michezo ya ligi kuu  na kesho wata endelea na mazoezi na mechi ya ijayo watacheza na Afrikan Sport. 

No comments