Ads

REA YALIA NA WALA RUSHWA KATIKA MIRADI YAKE


Na John Luhende
mwambawahabariblogspot.com
Kutokanana kuwepo kwa  malalamiko kuhushusu rushwa  katika  utoaji huduma wa umeme Wakala wa  nishati vijijini (REA) imewahimiza wananchi kuwa  makini na kuwaagiza maliipo    yo yote yanayohusuyo huduma  yafanyike katika ofisi za TANESCO  pekee nakutolewa stakabadhi , naiwapo kutakuwa na mazingira ya  rushwa watoe taarifa maramoja kwa vyombo vya dola.

 Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi  mkuu   wa wakala wa nishati vijijini  Lutengano  Mwakahesya,  amewaonya wakandarasi wote  kutojihusisha na vitendo vya    rushwa  kuhakikisha  wanadhibiti   wakandarasi wadogo wafanyakazi na vibarua wao kutojihusisha na vitendo  vya rushwa na watakao shindwa kutetekeleza agizo hilo mikataba ao itasitishwa nawatanyimwa fursa ya kushiriki katika  zabuni za miradi mingine ya kusambaza umeme vijijini.

Pamoja na hayo   amengeza  kuwa,  idadi ya wateja walio unganishwa vijijini  imefikia 55,400  sawa na asilimia 22 ya matarajio ya kuunganisha wateja 250,000 na utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi   wa kupeleka umeme vijijini umekamilika kwa asilimia 83 na imefanya kufika vijiji  5,009  Tanzania bara  sawa na asilimia 33  hadi sasa ambapo  malengo ni kufikia vijiji5,336 na vijiji vilivyo baki  kufikiwa ni   10,058    ambapo uhitaji wa fedha ni mkubwa  ili kweza kukamilika kwa  mradi huo.

No comments