SERIKALI YA MAGUFULI YAVUNJA RECODI YA UKUSANYAJI MAPATO
mwambawahabariblogspot.com
SHILINGI bilioni 18.77 zimetumwa
kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini
kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.
Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za
Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na
bilioni 3 kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika
Halmashauri zote hapa nchini.
Dk.Mipango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na
wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika
kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.
Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu
wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini
waweke wazi matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila
shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.
Post a Comment