RAIS WA TAHILISO AWAANGUKIA WENYE NYUMBA KUHUSU WANAFUNZI
RAIS wa
Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHILISO), Geofrey
Kiliba , amewataka watendaji wa vyuo vya elimu ya juu kuhakikisha wanafunzi
waliomaliza ngazi ya diploma wanapata namba za uthibitisho (AVN) kwa wakati ili
kuwawezesha kuendelea na masomo ya shahada bila vikwazo.
Akizungumza
na waandishi wa habari,Jijini Dar es Salaam amesemakiliba amesema jumuiya hiyo inasikitishwa na ucheleweshaji wa
upatikanaji wa namba hizo, ambao umesababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa
kuendelea na masomo yao kwa wakati, licha ya kutokuwa na makosa katika kutimiza
masharti yanayohitajika.
Amesema
ucheleweshaji huo unaweza kuathiri juhudi zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya
Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha elimu ya juu,
ikiwemo uwekezaji katika mikopo ya ada na fedha za kujikimu, ujenzi wa kampasi
za vyuo katika mikoa mbalimbali, uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia na
ujenzi wa hosteli za wanafunzi.
"Naiomba Taasisi na watendaji wa vyuo husika kuchukua
hatua za haraka kushughulikia changamoto za wanafunzi waliokwama kupata namba
hizo, akisisitiza kuwa jukumu hilo ni la vyuo na watumishi wenye dhamana badala
ya kuwaachia wanafunzi kubeba mzigo huo"amesema
amewaomba wamiliki wa nyumba na hosteli zinazopangishwa kwa wanafunzi kuzingatia hali ya maisha ya vijana hao na kuepuka kuongeza kodi kwa viwango vinavyoweza kuwaathiri katika safari yao ya elimu.
Amesema baadhi ya wamiliki wa nyumba wamekuwa wakipandisha kodi kutoka Sh70,000 hadi Sh100,000, hatua aliyodai kuwa inawaongezea wanafunzi mzigo wa gharama za maisha wakati wengi wao hawana vyanzo rasmi vya mapato.
Ameeleza kuwa baadhi ya wanafunzi wanaofika katika vyuo vya elimu ya juu hutegemea michango ya wazazi, walezi, ndugu na marafiki, huku wengine wakitoka katika familia ambazo zimeuza mali zao, ikiwemo mifugo na mashamba, ili kuwawezesha watoto wao kupata elimu.
Kutokana na hali hiyo, amewasihi wamiliki wa nyumba kuwa na huruma na kuwapa wanafunzi mazingira yanayowawezesha kuendelea na masomo yao bila kukabiliwa na changamoto kubwa za gharama za makazi.
Amesema ameamua kuanza kwa kuzungumzia changamoto zinazowakabili wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu kabla ya kuzungumzia masuala mengine ya kisiasa na yanayohusu hali ya nchi.
Post a Comment