QUEEN MASANJA ATEULIWA BALOZI WA LP PADS, MARTIN KADINDA ATOA DIRA YA KAMPUNI
Dar es Salaam
Kampuni ya LP PAD Trading Co. Limited imetangaza rasmi kuanza kupatikana kwa bidhaa zake za taulo za kike za LP PADS nchini Tanzania, huku ikimtambulisha msanii na mrembo maarufu Queen Masanja kuwa balozi mpya wa bidhaa hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa LP PAD Trading Co. Limited, Martin Kadinda, alisema kampuni hiyo imekuja na dhamira ya kuhakikisha wanawake na wasichana wa Tanzania wanapata taulo za kike zenye ubora wa hali ya juu kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
Kadinda alisema LP PADS ni bidhaa inayolenga kuchangia afya na usafi wa hedhi kwa wanawake na wasichana, huku kampuni hiyo ikijipanga kusambaza bidhaa zake katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwafikia walengwa wengi zaidi.
Aidha, alisema uteuzi wa Queen Masanja kama balozi wa LP PADS umetokana na ushawishi wake mkubwa kwa jamii, hususan kwa mabinti na wanawake, jambo ambalo litasaidia kufikisha ujumbe wa bidhaa hiyo kwa watu wengi zaidi.
Kwa upande wake, Queen Masanja alisema anafurahi kuaminiwa na LP PAD Trading Co. Limited na kupewa jukumu la kuwa balozi wa bidhaa hiyo.
"Ninafuraha kuwa sehemu ya safari hii muhimu ya kuhamasisha afya, usafi na ustawi wa wanawake na wasichana wa Tanzania. Ninaamini LP PADS zitasaidia wanawake wengi kupata taulo za kike bora kwa bei nafuu na kwa urahisi," alisema Queen Masanja.
Sambamba na uzinduzi huo, Martin Kadinda alitangaza fursa kwa mawakala wa biashara, wasambazaji na wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali kushirikiana na kampuni hiyo katika kusambaza LP PADS nchini kote.
Alisema kampuni hiyo pia imejipanga kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kuendelea kutoa ajira kupitia shughuli zake za usambazaji, masoko na mauzo, huku ikisisitiza kuwa upatikanaji wa taulo bora za kike ni haki muhimu kwa kila mwanamke na msichana.
Uzinduzi huo unaashiria hatua mpya kwa LP PAD Trading Co. Limited katika juhudi za kuboresha afya ya hedhi na ustawi wa wanawake nchini Tanzania.


Post a Comment