USIKU WA "KNOCK OUT YA MAMA" MSIMU WA 5 KUWEKA HISTORIA,
Na Mwandishi wetu-Dar es salaam
MSIMU wa Tano wa pambano kubwa la Knockout ya Mama Masumbwi kuchuana vikali likalofanyika Julai 26, 2025 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuweka historia kwa kuwa la mapambano nane ya kuwania mikanda kiwemo ya WBO na WBC.
Akizungumza na waandishi wa habari Juali 23, 2025 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Matangazo na Uzalishaji kutoka Kampuni ya Mafia Promotion Omari Clayton pambano hili litakuwana jumla ya mapambano 10 yakihusisha mabondia wa kimataifa la viwango vya juu.
Mapambano nane yatakuwa ya mikanda na lengo ni kufanya "boxing" ya Tanzania iende mbali kimataifa. Bondia atakayeshinda atapata fedha, mkanda na nyota, hivyo kutambulika kimataifa," amesema Clayton.
Usiku wa siku hiyo ya pambano utakuwa ni siku ya mtoko kila Mtanzania aweze kuifanya Julai 26, 2025 kuwa siku ya Mtoko kwa kwenda kushuhudia pambano hilo.
Kwa upande wake Promota Jay Msangi amewasifia na kuipongeza Mafia boxing promotion kwa kuandaa pambano kubwa linalojulikana kama "Knock Out ya mama." amesema Clayton.
Ameongeza kwa kusema kuwa uwekezaji waliouweka Mafia boxing promotion ni takribani bilioni mbili na ni uwekezaji mkubwa sana. Kwamba mapambano yanayokuja makubwa ya ubingwa ni WBC, WBO, na UBO yote yatafanyika nchini.
Naye Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion Ally Zayumba akieleza maandalizi ya mwisho kuelekea usiku wa Knockout ya Mama Season 5. Ameeleza kuwa kila kitu kipo tayari, na mashabiki wajiandae kushuhudia burudani ya kipekee isiyopimika.
Post a Comment