Ads

AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAWEKA TABASAMU KITUO CHA KULELEA WATOTO -CHAKUWAMA SINZA

Akiba Commercial Bank Plc imeguswa kuendelea kuunga Mkono jamii kwa kutoa  msaada  wa mahitaji mbalimbali katika kituo cha kuelelea Watoto Yatima kilichopo Sinza Dar es Salaam.

Amebainisha hayo Machi 28,2025  Dar es salaam Bi Dora Saria, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Bank, wakati akikabidhi msaad kituo cha kulea Watoto  cha Chakuwama, ikilenga kuboresha ustawi wa watoto na kuleta tabasamu kwenye nyuso zao.

Bi. Dora amesema Msaada huo, ambao umetolewa  ni mahitaji muhimu, unaonesha dhamira ya Benki hiyo ya kusaidia watu wenye uhitaji na kujenga  matumaini kwa mustakabali mwema alieleza na wana inaamini katika kuunga mkono jamii na kuleta mabadiliko chanya ya kudumu

"Akiba Commercial Bank, tunaamini katika nguvu ya mshikamano kwa kubadili maisha. Msaada huu ni hatua muhimu ya kuhakikisha ustawi wa watoto hawa na kuleta matumaini kwa wenye uhitaji kwa maisha bora yajayo," amesema Bi. Saria.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa kituo hiko cha Chakuwama  Hassan Tabu, ameshukuru sanaa  Akiba Commercial Bank kwa ukarimu wao, amesema  kuwa msaada huo ni  mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya watoto hao.

"Tunaishukuru sana Akiba Commercial Bank kwa kusimama nasi katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na Kwaresma kwani kutoa ni Moyo wala si utajiri waendelee hivyo hivyo na Mungu awabariki " ameshukuru Hassan

Aidha Msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watoto na kuwapatia sababu ya kutabasamu.


Kupitia juhudi hizi, Akiba Commercial Bank Plc inathibitisha tena dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii kwa vitendo, ikilenga kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu kwa jamii inayoihudumia.

No comments