Ads

AKIBA COMMERCIAL BANK PLS YAWATOA HOFU WATEJA WAKE KARIAKOO

Akiba Commercial Bank  imeendelea kujitoa si tu kuhudumia wateja wake bali pia kushiriki katika juhudi za kijamii wakati wa dharura na majanga, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kujenga jamii imara na yenye mshikamano




Ameyasema hayo  leo Novemba 17 ,2024 Jijini Dar es salaam na  Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt. Tobha Nguvira, ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha maafa  Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kupokea msaada kutoka Akiba Commercial Bank walipokuja kutembelea  eneo la ajali la jengo la biashara lililoporomoka Kariakoo, ajali  iliyosababisha madhara makubwa, ikiwemo  majeruhi, uharibifu wa mali  na wengine kuangamia

"Tunashukuru sana Benki hii imetoa msaada wa katoni  kadhaa za maji kwa ajili ya kusaidia  timu ya uokozi inayofanya juhudi kubwa za kuokoa watu waliokumbwa na ajali hiyo mbaya na ya kusikitisha na wamekuja na  Ujumbe wa Akiba Commercial Bank uliongozwa na wafanyakazi wa matawi ya Kariakoo pamoja na makao makuu , akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Bi. Dora Saria, na Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji, Dkt. Danford Muyango." amesema Dkt Nguvira

Naye  Kaimu Afisa Biashara Mkuu Dkt. Danford Muyango amesema Akiba  Commercial  imewaomba wateja wake  ambao  wameathirika na janga la kuporomoka gorofa kariakoo kufika kwenye matawi   kutoa taarifa za athari walizopata kwani  benki itatoa usaidizi wa tathmini wa kina kuhusu huduma za bima na kuanzisha utaratibu wa marejesho ya mikopo yao kulingana na hali yao .


No comments