WANANCHI DODOMA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA
Na Mwandishi wetu Dodoma
Mkoa
wa Dodoma unatarajia kuanza uboreshaji wa daftari la Kudumu la mpiga
kura tarehe 25 septemba 2024 hadi tarehe 1 octoba 2024.
Uboreshaji
huo ni sehemu muhimu ya mchakato wa uchaguzi na utahusisha kurekebisha
taarifa waliokosa sifa,mfano waliofariki, waliofungwa kifungo cha zaidi
ya miezi sita na waliopata changamoto ya afya ya akili ili kuhakikisha
kuwa wapiga kura wote wanawezae kijiandikisha na kuhakiki taarifa zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameyabainisha hayo leo katika
mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema ni muhimu wapiga kura
kuhakikisha kuwa wana taarifa sahihi ili waweze kutimiza haki yao ya
kikatiba katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025.
RC Senyamule amesema
Dodoma inakadiriwa kuwa na wapiga kura 1,777,834 kati ya hao wapo ambao
hawajawahi kujiandikisha, idadi yao inakadiriwa kuwa 845,976.
"Hili ni kundi kubwa na ni kundi muhimu sana hivyo nawasihi kujitosheleza kujiandikisha" - RC Senyamule
Amesema
vituo vitakavyotumika katika uboreshaji ni majengo ya umma kama vile
ofisi za watendaji wa kata, ofisi za watendaji wa mitaa, ofisi za
wenyeviti wa vijiji, ofisi za wenyeviti wa vitongoji na shule katika
maeneo ambayo hakuna majengo ya Umma.
Aidha RC Senyamule amesema
vituo vimeshajengwa na vimewekwa alama ili wananchi waweze kuvitambua na
vituo hivyo ni Wilaya ya Dodoma vituo 429,Bahi 191, Kongwa 229 ma
Chamwino 805.
Hata hivyo wanaohusika na zoezi hilo ni wananchi ambao
1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea
2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu mwaka 2025
3. Waliojiamdikisha awali na wamehama kata au jimbo moja kwenda kingine.
4. Waliopoteza sifa mfano waliofariki kuondolewa kwenye daftari.
5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji.
6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Dodoma amesisitiza umuhimu wae mchakato huo na
amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ka
uboreshaji wa daftari la Kudumu la mpiga kura.
Post a Comment