Ads

MKURUGENZI WA FCC ATOA NENO KUHUSU BIDHAA BANDIA,AWAKARIBISHA SABASABA WAWEKEZAJI.

 

TUME ya Ushindani nchini (FCC) imesema itahakikisha Mwananchi nchini haumizwi na bidhaa zisizo na ubora ikiwemo kusimamia sheria ya ushindani nchini inayodhibiti bidhaa hizo.


Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa FCC, William Erio,wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la FCC lilopo kwenye maonesho ya 48 ya sabasaba yanayoendelea jijini hapa.

Erio amesema FCC imejitahidi kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya kuepuka Bidhaa Bandia.


Erio,amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kabla ya kufanya biashara nchini watembelee FCC kwa lengo la kupata elimu .


Hata hivyo,Erio,amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji kutokana na sera nzuri ikiwemo kuwepo kwa mamlaka inayodhibiti bidhaa bandia ikiwemo FCC.

No comments