Home
/
Unlabelled
/
Wananchi Watakiwa kutumia Huduma ya TAKAFUL LTD ambayo ni huduma ya bima yenye misingi na Sheria za kiislam
Wananchi Watakiwa kutumia Huduma ya TAKAFUL LTD ambayo ni huduma ya bima yenye misingi na Sheria za kiislam
Na Francisco Peter, Dar es Salaam.
Watanzania wametakiwa waweze kuchangamkia kujiunga na huduma za bima kwani zinasaidia kutatua changamoto wanazoweza kukumbana nazo wakati wanapokubwa na majanga ya aina mbali mbali.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa TAKAFUL inayotolewa kupitia kampuni ya uwakala ya GALCO Insurance kwa kushirikiana na kampuni mama ya ZIC TAKAFUL LTD ambayo ni huduma ya bima yenye misingi na Sheria za kiislam .
Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Bima nchini (TIRA) Bi.Khadija Said aliyasema hayo alipo fika kwenye hafla hiyo kumwakilisha Kamishina wa bima wa TIRA nchini Dkt.Baghayo A.Saqware ambapo amezitaka wakala zinazotoa huduma za bima kutoa huduma hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizotolewa na mamlaka hiyo.
Bi . Khadija amesema kuwa kampuni zote za uwakala wa bima zinapaswa kuzingatia kanunu na sheria zilizowekwa na TIRA iliwaweze kitoa huduma kwa wateja wao kwa kiwango na ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha ameendelea kufafanua kuwa kwa mujibu wa mpango wa kuendeleza sekta ya fedha hadi kufikia mwaka 2030 matumizi ya bima yamelengwa kufikia asilimia 50 lakini mpaka sasa matumizi hayo ni asilimia kumi na tano pekee nakwamba uelewa wa matumizi ya bima umelengwa kufikia asilimia 80 mwaka 2030 ambapo kwa sasa .
Hata hivyo Bi. Khadija amezisisitiza kampuni na wakala za bima kuendelea kutoa elimu kwa watanzania waweze kuchangamkia.
"Huduma hii ya Bima ya Takaful mchakato wake umeanza rasmi mwaka 2008 kupitia kampuni ya ZIC Insuarance na imezinduliwa rasmi miezi mitatu iliyopita na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi,hatua hii ni kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya Bima ya Misingi ya hesheria ya kislam TAKIFUL lakini huduma hii inatolewa kwa waislam na wakristo kwa ujumla"amesema
Takaful ambayo inasimama kama nguzo katika jamii na inasimama katika misingi ya kushirikiana pale ambapo kutakuwa na majanga au faida.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa makampuni ya GSM Group yanayomiliki kampuni ya Galco Insuarance Ltd ,Benson Mahenya amesema huduma zao za bima ya Takaful sio sera ila ni ahadi ya kuwa wapo karibu na watu katika kutatua changamoto za kibiashara na kimaisha kiujumla .
"Tunafanya kazi katika misingi ya kweli na uwazi na kuhakikisha usawa katika utoaji wa huduma,tuna uzoefu wa miaka mitano sokoni na katika kipindi hiki tumeweza kutoa huduma kwa watu binafsi zaidi ya mia tano na makampuni zaidi ya kumi ,"amesema Mahenya .
Naye meneja Biashara Emmanuel Bugabu amesema kuwa Galco Insurance Brokers inashirikiana na makampuni mbali mbali ya kiwemo MAYZUH COMPAZNY LIMITED ilikutoa mafunzo kwa wafanyakazi na kuhakikisha wana uelewa na huduma ya Takaful na wanashirikiana na pia na ZIC TAKAFUL LTD katika utoaji huduma hiyo ya bima ya misingi ya kiislam TAKAFUL.
"Nia yetu ni kukuza mwamvuli wetu wa huduma za bima kwa watu wote wakiwemo mtu mmoja mmoja , wanafamilia,wafanyabiashara na makampuni au taasisi mbali mbali,nakusisitiza kuwa wafanyakazi wa Galco Insuarance wamepata elimu ya kutosha kutoa huduma kwa wateja" amesema Bugabu
Post a Comment