TEMDO NA MAPINDUZI KATIKA TEKNOLOJIA YA MASHINE NCHINI.
Afisa Masoko wa (TEMDO), Dkt.Sigisbert Mmasi akionesha kitanda cha kujifungulia akinamama wajawazito ((Delivery bed bed )kitanda hicho kimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kinaweza kushuka na kupanda kulingana na mahitaji ya muhusika.
Na. Mwamba wa habari
Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) imeendelea kuleta mapinduzi makubwa katika teknolojia ya mashine na bunifu mbalimbali ikiwemo vifaa vya hospitali.
Bunifu hizo zimekuwa zikisaidia katika huduma mbalimbali kulingana na mahitaji kwa wakati na kile ambacho anakihitaji mteja ,mashine kama vile Grape Crusher Destemmer na kitanda cha kujifungulia mama mjamzito ((Delivery bed ) vimeleta vimeleta hamasa kwa wabunifu na wahandisi nchini.
Akizungumza na Mwamba wa habari , Afisa Masoko wa (TEMDO), Dkt.Sigisbert Mmasi alisema wameamua kuwasogezea wajasiriamali mashine za kuchakata zabibu kwa ajili ya viwanda vya "wine" kwani mashine hiyo itamuwezesha kuchakata zabibu takribani kilo 700 kwa saa moja.
Aidha aliongeza kuwa TEMDO wana mashine mbalimbali za kilimo kama vile mashine ya kukamua mafuta ya alizeti au ufuta zinaziweza kukamua kilo elfu 3 kwa siku pamoja na mashine za kuchakata mihogo Tani 12 kwa siku moja hata kama muhogo unatoka shambani.
Alisema TEMDO imelenga katika ukuzaji wa thamani wa mazao ya kilimo hivyo imejikita katika uzalishaji mkubwa,kwa wakulima wanao weza kununua mashine kwa vikundi wataweza kumiliki mashine kwa ajili ya uzalishaji.
''Mashine hizi pia hata mtu binafsi naye anaweza kununua". Alisema
Amesema kwa upande wa sekta ya afya amesema wamepata ithibati ya vifaa tiba vya aina kumi na saba , wamekwisha andaa vifaa tiba vya aina Saba ambavyo viko tayari,kitanda cha mgonjwa, kiteketezi taka za taka za hospitali ambacho hakina madhara ya kikemikali kwa binadamu.
TEMNDO pia inatoa Mafunzo ya uhandisi viwandani kwa wahandisi na mafundi kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa uzalishaji ambapo ofisi zao zipo mkoani Arusha .
Post a Comment