YANGA YAVUNA PESA YAMPIGA BEI FEITOTO
Klabu ya soka ya Yanga imetangaza kumuuza mchezaji wake Feisal Salum Abdallah (FEI TOTO) kwa dau ambalo halijawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
Taarifa rasmi ya klabu ya soka ya Yanga imeeleza kuwa, ilipokea maombi kutoka klabu ya Azam ya kutaka kumnunua mchezaji huyo na baada ya mazungumzo ya pande zote mbili Yanga imekubali kumuuza mchezaji huyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Feisal ataungana na timu yake mpya mara baada ya kumalizana kuhusu maslahi binafsi na dirisha la usajili kufunguliwa.
Yanga imemtakia heri mchezaji huyo ambaye awali aligoma kurudi kuichezea klabu hiyo na hajacheza Yanga tangu mwaka huu uanze.
Post a Comment