Ads

Jumla ya shule 811 zimefikishiwa Vifaa vya TEHAMA



 Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unatarajia kutumia shilingi 575,000,000 ,kwa ajili ya Mradi wa Kupeleka Vifaa Maalum vya TEHAMA vya Kujifunzia kwa Shule 16 Zenye watoto wenye mahitaji maalum hapa nchini.



Shule hizo zitakazonufaika ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Mpwapwa (Mpwapwa-Dodoma), Sekondari ya Mkolani (Mwanza), Sekondari ya Kashaulili (Mpanda-Katavi), Sekondari ya Morogoro (Morogoro), Sekondari ya Shinyanga (Kishapu-Shinyanga), Sekondari ya Wavulana Songea (Songea), Sekondari ya Kazima (Tabora) na Sekondari ya Haile Selassie (Mjini Magharibi).


Hayo ameyasema mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote ( UCSAF)  Justina Mashimba  leo Februari 13,2023 Jijini Dodoma, wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo.


Amesema kuwa vifaa vitakavyopelekwa katika shule hizo ni pamoja na na TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu).


Pia Amesema kuwa  kuwa Jumla ya shule 811 zimefikishiwa Vifaa vya TEHAMA ambapo kwa wastani kila shule imepewa Kompyuta 5, Printa 1 na Projekta 1.

"Kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, Shule 150 zitafikishiwa vifaa vya TEHAMA,Bajeti yake ikiwa ni TZS 1,950,000,000/- na vifaa hivyo vitasaidia wanafunzi kusoma katika shule hizo 811" Amesema Mashimba

Akizungumzia hali ya Mawasiliano nchini Mashiba amesema kuwa Mwaka 2009 Population Coverage ya Huduma za Simu ilikuwa asilimia 45 (45%) wakati kwa sasa imeongezeka hadi kufikia asilimia 96 (96%),Teknolojia ya 2G coverage yake ni 96%,3G ni 72%,4G ni 55% na Geographical Coverage ya 2G ni 69%; 3G ni 55% na 4G ni 36%.

Kwa upande wa Ujenzi wa Minara Vijijini Mtendaji huyo amesema UCSAF imeingia mikataba kufikisha huduma katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654, Wakazi 15,130,250 ambapo Minara 1,087 yenye vijiji 3,378 na wakazi 13,320,750 na Utekelezaji unaendelea katika Minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi 1,809,500 kwa ruzuku iliyotolewa yaTZS bilioni 199 ikiwemo pia Mradi wa kimkakati wa Zanzibar, Minara 42, Shehia 38 ruzuku TZS bilioni 6.9

No comments