TUNDU LISU AWASILI NCHINI ,MAMIA WAJITOKEZA KUMLAKI
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amewasili nchini akitokea Ubelgiji baada ya kuishi nchini humo tangu mwezi Novemba mwaka 2020.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam, Lissu amepokelewa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA pamoja na wanachama wa chama hicho.
Hata hivyo, Jeshi la polisi limeimarisha ulinzi na kuhakikisha wafuasi hao hawaingii ndani ya eneo la uwanja na badala yake wanabaki nje ya lango kuu pembezoni mwa barabara ya Nyerere.
Lissu alitangaza uamuzi wake wa kurejea nyumbani baada ya rais Samia kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa mwezi huu.
Post a Comment