RC SINYAMULE AWATAKA WANAFUNZI ,WAZAZI KUTAMBUA UMUHIMU WA MAZINGIRA
Mkuu wa mkoa wa dodoma Rosemary Sinyamule amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni mara baada ya shule kufunguliwa.
Senya Mule ameyasema hayo katika ziara ya Kampeni ya upandaji wa miti iliyofanyika katika hospital ya wilaya ya chemba jijini dodoma ambapo pia amewasihi wananchi kupanda miti Kurudisha uoto wa asili Ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Sinyamule amesema kuwa zipo Sheria ambazo inalazimika kufuatwa kuhakikisha kuwa mtoto anapata haki yake ya kwenda shule hivyo inapaswa wazazi na walezi watambua lengo na makusudi ya serikali ya awamu ya sita kwa watoto wa kidato Cha kwanza.
Aidha amesema kuwa yapo maelekezo ambayo yametolewa na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa ,hivyo ni jukumu la kila mwanafunzi kuwa na mti wake shuleni ambao atautuza kwa kipindi chote awapo shuleni na wazazi watambue kama elimu ya vitendo.
Post a Comment