MJEMA AINGIA KAZINI
DAR ES SALAAM
Mwamba wa habari
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Edward Mjema amewataka watumishi waliko chini ya ofisi yake kutekeleza majukumu yao kwa bidii, umoja, ubunifu na wakati wote kuhakikisha wanakuwa mfano bora.
Mjema ameyasema hayo leo wakati akizungumza na katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam leo.
Aidha Mjema amewataka watumishi hao kuendelea kujenga, kutunza na kulinda haiba nzuri ya CCM na Mwenyekiti wake Rais Dakta Samia Suluhu Hassan.
Amewaambia kuwa kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuendelea kuyasema mazuri yanayofanyika kwa wananchi ili wayafahamu, kueleza uzuri wa CCM, kuwasikiliza wananchi kero au changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.
Ndugu Mjema amewasisitiza kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuendelea kuwajengea uwezo wanachama na viongozi wao kupitia mafunzo.
Post a Comment