MBINU ALIZO ZITUMIA RAIS SAMIA KUONGEZA WATALII WANAOPITIA KIA
Na.wellu Mtaki, Dodoma
Abiria 654,159 wameongezeka mwaka 2021/2022 sawa na 88% kutokana na Juhudi za rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan za kuitangaza inchi pamoja na vivutio vilivyomo kupitia filamu maalum ya Rayal Tour.
Hayo yamesemwa na mtendaji makuu wa kampuni ya uendelezaji na uendeshaji wa kiwanja cha ndege cha kilimanjaro ( KIA ) wakati akizungumza na wahandishi wa habari jijini dodoma kuhusu taarifa ya utekelezaji wa shughuli za KADCO .
Amesema kuwa mafanikio mengine ni kupitia shirika jipya la ndege la Eurowings Discover(part of Lufthansa Group)iliyoanza safari zake kutoka Frankfurt,Ujerumani kwenda KIA kuanzia mwezi Juni mwaka huu,shirika hilo limechangia kuongeza idadi ya abiria na mizigo.
Aidha amesema katika kipindi cha uviko 19 shughuri za endeshaji KIA zilishuka kwa kiasi kikubwa kutokana na nchi nyingi kufunga anga ikiwa ni njia moja wapo ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo,hii ilipelekea idadi ya abiria kushuka kwa kiwango kikubwa kutoka laki 794,337 mwaka 2019/20 hadi kufikia abiria laki 347,757 katika kipindi Cha mwaka 2020/21 ikiwa ni punguzo la abiria kwa asilimia 56.
Kupunguza kwa shughuli za uendeshaji KIA kuliathiri mapato,ikizingatiwa kwa chanzo kikuu Cha mapato ya KADCO ni tozo zinazotokana na abiria wanaopita KIA pamoja na kutua na kuruka kwa ndege kiwanjani,hali hii ilipelekea menejimenti ya KADCO kuchukua hatua ya kubana matumizi na kusimamisha kwa muda baadhi ya shughuli za maendeleo ili iweze kupita Katika kipindi hiki kigumu ikiwa inaendelea kujiendesha,
Pia ameeleza kuwa Usafiri wa anga ni chachu ya kuwezesha kukua kwa sekta nyingine mtambuka ikiwemo sekta ya Utalii, mifugo,kilimo na biashara ambapo huimarisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia mnyororo wa thamani unaotokana na shughuli za uendeshaji wa KIA,mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo hupitia KIA kwa ajili ya kwenda kwenye masoko ya nje ya nchi,hii inafaida kubwa katika uchumi wa kanda ya kaskazini na Taifa kwa ujumla.
Post a Comment