Ads

BUDGET YA SH BILLION 751 ZA TOLEWA KWAJILI YA SEKTA YA KILIMO.

 


Na wellu Mtaki. DODOM

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dodoma na ni mkulima Mariam Ditopile ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kufanya mageuzi makubwa ya kilimo inchini kwa kutoa budget ya sh billion 751 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 uku billion 631 zilielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.


Ameyasema hayo  jijini Dodoma wakati wa Mkutano wake na wandishi wa habari ambapo amesema kwa kipindi kifupi cha Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan mageuzi makubwa yamefanyika katika sekta ya Kilimo kulinganisha na miaka ya nyuma.


Mbuge Ditopile ameongeza kuwa ongezeko la Bajeti ya Kilimo kwa mwaka huu wa fedha ni takribani asilimia 300 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2020/21 ambapo kiasi kilichotengwa ni Sh Bilioni 229 na kati ya fedha hizo ni Sh Bilioni 150 pekee ndio zilienda kwenye miradi ya maendeleo.


” Rais Samia pia amejidhatiti kwenye eneo la tafiti za Kilimo, Bajeti ya tafiti za Kilimo imepanda kutoka Sh Bilioni 7.3 kwa mwaka 2020/21 hadi Sh Bilioni 40 kwa mwaka huu wa fedha. Tunamshukuru Rais pia kwa kupandisha bajeti ya Uzalishaji mbegu kutoka Sh Bilioni 5.4 hadi Sh Bilioni 43 kwa mwaka huu wa fedha 2022/23.


Pia tumeshuhudia utaratibu mzuri wa kuwawezesha wakulima nchini kupata Mbegu za Alizeti ambapo gharama zote ni Sh 3,500 tofauti na bei ambayo haikua na ruzuku ambayo ilikua ni kSh 7,000 hadi 8,000,” Amesema Mbunge Ditopile.


Amesema kwa namna ambavyo Rais Samia ameonesha mageuzi makubwa kwenye sekta ya Kilimo wao kama Wakulima wanampongeza Rais Samia kwa jitihada za dhati za kuwakomboa Wakulima kwani ni wazi mchango wa mbolea ni mkubwa katika sekta ya Kilimo hususani katika kuongeza tija.


” Tunamshukuru Rais Samia na Serikali yake kwa usikivu wao kwetu sisi Wakulima kwa kutuletea mfumo mzuri wa Mbolea ya Ruzuku pamoja na kutoa kipaumbele kwa wazalishaji wa ndani ili kulinda viwanda vyetu, ajira na Usalama wa chakula


Serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa ya kuvutia wawekezaji ambapo sasa tunashuhudia ujenzi mkubwa wa kiwanda cha Mbolea cha Intracom Fertilizer kinachojengwa jijini Dodoma na mwekezaji kutoka Burundi, uwekezaji wa kiwanda hiki utatoa ajira zaidi ya 3000 kwa watanzania,” Amesema Ditopile.


Aidha amewasihi wananchi wajitokeze kuhesabiwa Agost 23, na kuwataka wakulima wote inchi kutoa ushirikiano wa kutoa Taarifa zilizo za kweli kama ni wakulima Ili kupata data ambazo zitasaidia kuleta maendeleo kwenye sekta yetu ya kilimo.

No comments