Ads

PROFESA NDALICHAKO KWA KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI WA NSSF, PSSSF WALETA MATUMAINI MAPYA MAFAO YA WASTAAFU .

 Na Francis Peter, Dar es Salaam

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wastaafu katika kuhakikisha wanapata mafao yao kwa wakati kupitia mashariki ikiwemo NSSF na PSSSF.

Akizungumza leo tarehe 22/7/2022 jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wastaafu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali ipo tayari kuwasikiliza na kutatua changamoto mbalimbali ili wastaafu waweze kupata mafao yao.

Profesa Ndalichako amesema yupo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto zote ambazo ni kikwanzo katika kuhakikisha wastaafu wanalipwa kwa wakati.

"Ni muendelezo wa kukutana na wastaafu katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua changamoto zao" amesema Profesa Ndalichako.

Amesema kuwa tayari kazi imeanza tunawasikiliza na tunatatua changamoto na kama nilivyosema Wizara yangu pamoja na mambo mengine ina dhamana ya kusimamia wastaafu wanaolipwa mafao kupitia Mfuko wa NSSF na PSSSF.

Amesema kuwa wapo wastaafu ambao wanalipwa mafao yao kupitia hazina, hivyo wakifika katika mkutano wanapewa  kwa ajili ya kuzijaza na baadaye fomu hizo zitawasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

"Tunatatua changamoto moja kwa moja za wastaafu ambao wanalipwa kupitia Mfuko wa NSSF na PSSSF," amesema Profesa Ndalichako.

Profesa Ndalichako amefafanua kuwa anathamini mchango  uliotolewa na wazee wastaafu  katika ujenzi wa Taifa, serikali  itahakikisha kwa kushirikiana na watendaji wa NSSF  na PSSSF changamoto zao zinapatiwa majibu rafiki.

Hata hivyo amebainisha kuwa miongoni mwa changamoto za wastaafu aliokutana nao ni pamoja na mapunjo ya mafao, huku akisisitiza kuwa zote zitapatiwa ufumbuzi na kila mstaafu atapata huduma anayostahiki

Waziri Profesa Ndalichako leo amekutana na wastaafu zaidi ya 1,000 wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wana hudumiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PSSSF.

No comments