Ads

AJIRA ZA MAKARANI WA SENSA ZISITOLEWE KWA KUJUANA

 

Na Nasra Rajabu

Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,akizindua rasmi nembo ya Sensa ya makazi ya watu pamoja na kutangaza tarehe 23 ya mwezi wa nane kuwa ni siku ya kuhesabiwa.

Ndugu mhariri Katika hotuba yake Rais Samia aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo kwa sababau bado zipo jamii zinazoamini kwamba kuhesabiwa ni kitu cha laana jambalo ambalo siyo kweli.

Sote tunafahamu kwamba zoezi hilo linafanyika kila baada ya miaka kumi hivyo ni kweli kabisa wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa siku hiyo kwa sababu Serikali ikishajua idadi ya watu wake inakuwa rahisi kupanga bajeti ya maendeleo.

Ndugu mhariri wakati zoezi la uzinduzi wa nembo hiyo Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, Mama Anna Makinda akiwa jukwaani alieleza taratibu za ajira za makarani wa Sensa za mwaka huu zitakavyotolewa.

Alisema kama kuna watu walidhani wanaweza kuwaleta ndugu zao wasahau kwa sababu ajira hizo zitatolewa kidigitali na huko huko wanakoishi hao makarani,Lakini pia Anna Mkinda alitahadharisha sifa hizo sikitolewa basi zisikiukwe.

Ndugu mhariri ikumbukwe kwamba mwezi mmoja uliopita kulikuwa na zoezi la Anwani za makazi ambapo ajira za watu hao zinadaiwa kuwa na malalamiko makubwa kwa sababu wapo baadhi ya watu wamepeana kwa kujuana jambo ambalo ni baya sana.

Ni wazi kwamba asilimia kubwa ya ajira za anwani za makazi zimetolewa kwa kujuana aidha marafiki au ndugu kwa lugha ya mitaani inaitwa”Connection”ni jaambo ambalo limeumiza watu wengi mno.

Kwa ninavyofahamu miongoni mwa sifa za ajira zao ilitakiwa wachukuliwe wakazi wa sehemu husika lakini kwa asilimia kubwa inadaiwa baadhi ya watu wengi wameenda kufanya kazi katika maeneo ambayo hawayajui kabisa sasa hili lazima liangaliwe lisijetokea katika ajira za sensa.

Ndugu mahariri hata Rais Samia mara nyingi katika hotuba zake amekuwa akisisitiza kuajiri watu wenye sifa na siyo ajira za kindugu au kujuana ambapo ukifatilia ajira za kujuana hata katika mchakato wa ajira zake zinakuwa za muda  mfupi jambo ambalo ni baya sana kampuni au taasisi.

Ndugu mhariri Pamoja na kwamba ajira za makarani hawa zitatolewa katika makazi yao lakini wasimamizi wa ajira hizo wanatakiwa kutokuwa na upendeleo wowote kwa sababu hata ajira za anwani za makazi wapo baadhi ya watu hawajui hata kutumia simu janja na umri wao umeenda sasa hatuwezi kwenda kwenye kasi inayotakiwa.

Ngugu mhariri hili zoezi la Sensa ni kubwa mno linahitaji watu makini kwa sababu ukiwa ajiri watu wasiokuwa na vigezo kuna uwezekano mkubwa kupata idadi ya watu feki,Hivyo basi kauli ya Anna Makinda iendelee kusimamiwa vyema na baadhi ya viongozi ili tupate takwimu bora ambayo itatuletea maendeleo.

Ni matumaini yangu kwamba,Viongozi watalisimamia hilo kwa sababu itakuwa ni aibu kubwa kumwajiri mtu asiyekuwa na sifa wakati kuna watu wapo mitaani wamesoma na wanasifa lukuki,Lazima tubadilike.

Mwandishi wa maoni  hayo ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Tumaini Tawi la Dar es Salaam(TUDARco).

No comments