Ads

TAARIFA YA KUFARIKI KWA MSAIDIZI WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE

 









Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na aliyekuwa msaidizi wake Adam Issara (enzi za uhai wake)

Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete imethibitisha kutokea kwa kifo cha Katibu wa Rais Mstaafu, Adam Issara kilichotokea jana jioni Jijini Dar es Salaam.


Adam Issara alifariki akiwa katika Hospitali ya Dr. Mvungi jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ambapo taratibu za msiba na mazishi zitatolewa punde.

"Wakati wa uhai wake, Ndugu Adam Issara alikuwa Mtu mwaminifu, muadilifu, mchapa kazi hodari na nguzo muhimu ya Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kabla ya kujiunga na Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu mwaka 2017, Adam Issara alifanya kazi katika iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa Afisa Dawati katika Idara ya Asia na Australasia, na baadae kuwa Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kati ya mwaka 2007 na 2017"

"Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na familia yake wanaungana na mjane wa Marehemu, Bi. Happy Godfrey, familia ya Marehemu Adam Issara katika kipindi hiki cha simanzi na maombolezo, Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema, peponi" Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne

No comments