WASINDIKAJI NA WAJASIRIAMALI WA KOROSHO MKOA WA MTWARA WAPATIWA MAFUNZO YA UBORA WA VIWANGO
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa Wajasiriamali na
Wasindikaji wa korosho mkoani Mtwara ili kuwajengea uelewa kuhusu viwango
katika bidhaa zao.
Akizungumza mara baada ya
kufungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brigedia Jenerali Marco
Gaguti amesema wajasiriamali na wasindikaji wa korosho wasiopungua 40,
wanapatiwa mafunzo kwani wanafanya shughuli zao na tayari bidhaa zao zipo
kwenye soko ila hazijathibitishwa ubora na TBS.
Aidha amesema mafunzo
hayo ni njia muafaka wa kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea taifa
maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya viwanda,Kilimo,Biashara, Uvuvi na maeneo mengine mengi.
“Mafunzo haya yamekuja
kwa wakati muafaka ambapo Serikali imeazimia kwa dhati kabisa kuendeleza
viwango ili kutoa ajira katika kada mbalimbali pamoja na kuziwezesha bidhaa
zetu kushindana katika masoko ya ndani, kikanda na nje ya nchi”. Amesema
Mhe.Brigedia Jenerali Gaguti.
Amesema TBS inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na watendaji waliopo katika halmashauri zetu nchini ili kurahisisha kufikisha huduma kwa wananchi
Post a Comment