Ads

HOSPITALI YA RUFAA DODOMA YAANZA UFUAJI WA HEWA YA OKSIJENI



Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma imeanza Kufua Hewa ya Oksijeni ambapo ina uwezo wa kuzalisha Mitungi 250 hadi 300 kwa siku

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Best Magoma amesema wamesambaza mtandao wa hewa hiyo kwa kutumia mabomba katika Wodi ya Watoto, Upasuaji na ya Wagonjwa Mahututi (ICU)

Inaelezwa kuwa, uzalishaji umepunguza gharama za ununuzi wa Hewa katika Hospitali hiyo ikiwa ni moja ya maandalizi ya kipindi hiki cha  COVID19. Mara ya mwisho kupata Wagonjwa wengi wanaohitaji hewa ya Oksijeni ilikuwa ni wagonjwa 29 kwa wakati mmoja.

No comments