RAIS SAMIA SURUHU HASAN ATENGUA UTEUZI WA DC NA DED MORO
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya Bakari Msulwa pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro,Shaila Lukuba ambako Wafanyabiashara wadogo waliondolewa kwa nguvu hivi karibuni.
Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu kusimamia jambo hilo.
Amesema amesikitishwa na kitendo cha kuondolewa kwa nguvu kwa Wafanyabiashara hao, na kwamba kama ingekuwa ni lazima Wafanyabiashara hao kuondolewa ingetumika njia nyingine na si nguvu na kuharibu bidhaa zao.
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza uamuzi huo mkoani Mwanza wakati wa mkutano wake na Vijana wa Tanzania kupitia vijana wa mkoa huo.
Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Wafanyabiashara hao walitengewa eneo la mbali kwa ajili ya kufanya biashara zao na walipoona hakuna biashara waliamua kurudi maeneo ya mjini na ndipo walipoanza kuondolewa kwa nguvu.
Post a Comment