Rais Samia aagiza kusimamishwa uongozi wa soko la Kariakoo
Picha kutoka maktaba mtandao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza kusimamishwa kazi kwa viongozi wa soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam kupisha uchunguzi wa namna wanavyo endesha shuguli za soko hilo.
Ameeleza hayo katika ziara ya kushtukiza Sokoni hapo ambapo amezungumzia biashara kuchangamana kama Fundi cherahani kuwa katikati ya Wafanyabiashara wa vifaa vya Kilimo na wauza sumu za panya.
Aidha Rais ameonesha kutoridhishwa na hali ya Biashara ya Soko la Kariakoo na kuahidi kufanya tathimini ili kuweka mazingira katika hali nzuri.
Rais Samia yuko katika ziara ya siku moja Mkoani Dar es salaam
Post a Comment