Ads

JISOMEE DONDOO ZA BAJETI KUU 2021-2022 ,BAADHI YA MAMBO YANAYO GUSA MOJA KWAMOJA JAMII UKIWEMO WEWE

 



BUNGENI, DODOMA:Serikali imesema itafanya marekebisho kwenye Sheria ya kodi ya majengo sura 289 ili ukusanyaji wa kodi ya majengo ufanyike kwa kutumia mfumo wa ununuzi na utumiaji wa umeme kupitia mashine za Luku.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 10, 2021 na Waziri wa Fedha na Mpango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha bungeni bajeti kuu Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Amesema kila mita ya umeme ina uhusiano na mmiliki wa jengo au mtumiaji wa mita, na kwa kuwa sheria ya kodi ya majengo inataka kodi hiyo ikusanywe kwa mmiliki au mtumiaji wa jengo, hivyo anapendekeza kodi ya majengo ya kiwango cha Sh1,000 kwa mwezi kwenye nyumba za kawaida zenye mita moja na itakatwa kwenye ununuzi wa umeme Luku.

“Napendekeza kiwango cha Sh5,000 kwa mwezi kwa kila ghorofa au apartment zenye mita moja na itakatwa kwenye ununuzi wa umeme (Luku). Serikali itaweka utaratibu kwenye nyumba za kawaida na za ghorofa zinazochangia mita moja na zinazotumia mita zaidi ya moja,” amesema.

 Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema mlipuko wa  COVID19 umesababisha kutofikiwa kwa baadhi ya malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani hususan sekta za Utalii, Usafiri wa Anga na Uingizaji wa Bidhaa kutoka Nje

Pia, baadhi ya Mashirika na Taasisi zimeathiriwa zaidi na mlipuko huo na kupelekea kupungua kwa michango ya gawio kwenye Mfuko mkuu wa Serika

 Waziri Mwigulu Nchemba amesema Makadirio ya matumizi kwa mwaka 2021 yalikuwa Trilioni 34.88 ambapo Trilioni 22.10 ni matumizi ya kawaida na Trilioni 12.78 ni Matumizi ya Maendeleo

Amesema, "Katika kipindi cha Julai 2020-Aprili 2021, jumla ya Tsh. Trilioni 24.74 zimetolewa na kati ya kiasi hicho Trilioni 17.42 ni kwa matumizi ya kawaida ambayo yanajumuisha Trilioni 6.09 kwa ajili ya mishahara na Trilioni 4.49 kwa matumizi mengine na Trilioni 6.84 kugharamia Deni la Taifa"

Waziri wa Fedha amependekeza Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila Mwezi za Madiwani moja kwa moja kuanzia Mwaka wa Fedha 2021/22.

Amesema, "Madiwani wanafanya kazi nzuri sana ya kusimamia shughuli za Maendeleo kwenye Kata zetu. Hawa ni Wabunge wenzetu"

SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 ITAGHARIMU TSH. BILIONI 328.2

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Sensa ya Watu na Makazi ambayo imepangwa kufanyika Mwaka 2022 itagharimu Tsh. Bilioni 328.2

Asema kwa mara ya kwanza watakaofanya zoezi la Sensa hiyo watakuwa wanatumia vishkwambi (Tablets)

 TANZANIA  KUENDELEA KUKOPA

Waziri wa Fedha na Mipango amesema  ,Tanzania ina uwezo wa kuendelea kukopa kutoka ndani na nje ya Nchi ili kugharamia Miradi yake ya Maendeleo na pia ina uwezo wa kulipa mikopo hiyo punde itakapoiva.

Amesema hayo Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

VITAMBULISHO MILIONI 2.3 VYA WAJASIRIAMALI VILITOLEWA

Waziri wa Fedha amesema vitambulisho Milioni 2.3 vya Wajasiriamali vilitolewa ili kuwawezesha kuwa na mazingira rafiki ya #Biashara

Vitambulisho hivyo viliiingizia Serikali Tsh. Bilioni 46.71, ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/21 viliboreshwa kwa kuwekewa picha na jina


MSAMAHA WA VAT KWA VIFAA VYA KIDIGITALI

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema katika bajeti ya Mwaka wa fedha 2021/22 amependekeza kusamehewa kwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika bidhaa za Kidigitali.

Ametaja vifaa hivyo kuwa ni Simu janja, 'Tablets' na 'Modems' ili kuongeza idadi ya Watu wanaotumia Mtandao Nchini

BODA BODA  KUHUSU FAINI 

Napendekeza kupunguza adhabu zinazotolewa chini ya sheria ya usalama barabarani sura namba 168 kwa makosa ya pikipiki na bajaji kutoka shilingi 30,000/= za sasa hadi shilingi 10,000/= kwa kosa moja lengo la hatua hii ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa". Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha.

Napendekeza mwaka wa fedha 2021/2022 serikali kuanza kulipa posho ya madaraka shilingi 100,000/= kwa mwezi kwa kila Mtendaji wa kata kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokuwa yakitumika sehemu kulipa madiwani"-Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha.

Madiwani wenzetu wanafanya kazi nzuri sana za kusimamia shughuli za maendeleo kwenye kata zetu, hawa ni Wabunge wakaazi wa kwenye kata zetu ambao kila siku wako na Wananchi wetu kwenye kusimamia shughuli za maendeleo”


“Katika baadhi ya halmashauri Madiwani wamekuwa wakikopwa posho zao na wengine hufikia hatua ya kupiga magoti kwa Wakuruhenzi Watendaji ili walipwe,hii imekuwa ikipunguza ufanisi katika Halmashauri zetu kwa Madiwani wengi kufanya maamuzi yanayopendekezwa na Wakurugenzi Watendaji hata kama hayana maslahi kwa Taifa ili waweze kulipwa posho zao”


“Jambo hili limeongelewa kwa hisia kali sana na Waheshimiwa Wabunge hapa bungeni, Wabunge na Madiwani, napenda niwaeleze kuwa Mama yetu (Rais Samia) amesikia kilio chenu na alinielekeza mimi pamoja na Waziri wa TAMISEMI kulitafutia ufumbuzi suala hili”


“Napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za Waheshimiwa Madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa Halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato, Halmashauri 16 zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A) zitaendelea kutumia mapato yake ya ndani kulipa posho za Madiwani kupitia kwenye akaunti zao''


No comments