Jenerali Katumba Wamala anusurika kifo
KAMPALA,Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Flavia Byekwaso amesema watu waliojihami kwa silaha wamelimiminia risasi gari lililokuwa limembeba waziri wa Uganda katika tukio linalosemekana kuwa la jaribio la kumuua.
Shambulio hilo limemjeruhi kamanda huyo wa wa zamani wa jeshi nchini Uganda, Jenerali Katumba Wamala na kusababisha kifo cha mtoto wake wa kike na dereva wake.
Kituo cha televisheni cha NBS kimeripoti kuwa washambuliaji hao waliokuwa katika pikipiki walilimiminia risasi gari la Jenerali Katumba ambaye ni waziri wa kazi na uchukuzi, katika eneo la Kisaasi.
Picha zilisambaa mitandaoni zimemuonesha Jenerali Wamala akiwa mdomo wazi kutokana na mshituko pembeni ya gari lake, huku nguo zake zikiwa zimejaa damu.
Picha hizo pia zilionesha matundu ya risasi katika gari hilo.
kwa hisani ya DW
Post a Comment