BABA wa Taifa la Zambia Kenneth David Kaunda amefariki dunia
BABA wa Taifa la Zambia Kenneth David Kaunda amefariki dunia kwa maradhi ya Pneumonia akiwa na umri wa miaka 97, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Kenneth Kaunda 'KK' mwanasiasa na mpigania uhuru wa Zambia alikuwa Rais wa kwanza wa taifa hilo na kuliongoza kuanzia 1964 hadi 1991.
Kaunda alikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa taifa hilo kutoka kwa Waingereza.
Siku mbili zilizopita Kaunda alilazwa katika hospitali moja ya jeshi Mjini Lusaka na kuomba maombi kutoka kwa wananchi wa Taifa hilo kupitia taarifa iliyotolewa na wasaidizi wake.
Post a Comment