Ads

IGP SIRRO AWATAKA ASKARI POLISI KUTENDA HAKI

 


28/05/2021  DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka askari kuhakikisha wanaendelea kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kushirikiana nao katika kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.

IGP Sirro amesema hayo Dar es salaam, wakati akizungumza na baadhi ya wananchi  wa eneo la Kawe wilaya ya Kinondoni ambapo aliwataka wananchi kuacha kutoa rushwa kwani kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali hasa watendaji wa kata na wenyeviti wa serikali za mitaa kuwashirikisha wananchi katika vikundi ya ulinzi shirikishi ili maeneo yao yaendelee kuwa salama.

No comments