Ads

WATOTO WANAONYONYESHWA MAZIWA YA MAMA PEKEE BAADA YA KUZALIWA NCHINI NI ASILIMIA 58

Mwambawahabari
Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania(TFNC), Bi Sikitu Simon Kihinga akitoa mada   jijini Dar es Salaam katika semina na waandishi wa habari.
..........................................................
Na Maria Kaira,Mwambawahabari
Takwimu za hali ya ulishaji watoto nchini zinaonyesha idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee nchini bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vyengine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe (TFNC) Sikitu Simon Kihinga Wakati akizungumza na wanahabari katika Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji wa Maziwa  ya Mama Duniani mwaka 2020 ambayo hufanyika kila Agosti 1-7 ya kila mwaka.

Ambapo alisema  watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi
katika kipindi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 53.

Bi . Sikitu amesema Idadi ya watoto wanaoanzishiwa vyakula vya nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 87.

“idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6 – 23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni asilimia 35 Vigezo hivyo ni idadi sahihi ya milo anayopewa mtoto kwa siku kulingana na umri wake, na mlo uwe na mchanganyiko wa vyakula kutoka kwenye makundi yasiyopungua manne ya vyakula,” amesema.

Amesema Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani kwa mwaka 2020 yamebebwa na kauli mbiu inayosema “Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira.

Amesema ili kuboresha viwango vya unyonyeshaji na ulishaji watoto vyakula vya nyongeza ,kila mmoja ana wajibu wa kufanya jambo Fulani katika azimio la Inocenti la mwaka 1990 nchi zilikubaliana mambo mbalimbali ya kuyasimamia makubaliano.

Amesema kauli mbiu hii inalenga kutukumbusha mchango wa unyonyeshaji katika utunzaji wa mazingira ya dunia na ikolojia yake sanjari na kulinda afya ya binamu.

Amesema kauli mbiu hii inahimiza jamii kuboresha kasi ya unyonyeshaji sanjari na kupunguza kiwango cha matumizi ya maziwa na vyakula mbadala vya watoto wachanga na wadogo.

“Aidha tukumbuke kuwa matumizi ya maziwa na vyakula mbadala vya watoto wachanga na wadogo yanakwenda sanjari na matumizi ya vifungashio mbalimbali vikiwemo vya plastiki, nishati ikiwemo kuni na mkaa, maji, chupa za kulishia watoto na ongezeko la hewa ya ukaa inayoathi
Kadhalika wataalam hao wa lishe walieleza kwamba mama anapomnyonyesha mtoto mfululizo kwa miezi sita ya mwanzo humsaidia kutopata mtoto mwingine mapema na pia humsaidia mtoto katika kuimarisha hatua mbalimbali za ukuaji.

Elimu hii ya unyonyeshaji iligusia pia mambo ya kuzingatia wakati wa kunyonyesha ambayo yalikuwa ni kwamba mama anatakiwa kuwa msafi (kwa nguo alizovaa na mwili wake) kwani asipozingatia usafi anaweza kumsababishia mtoto magonjwa, mtoto anatakiwa kunyonyeshwa katika hali ya utulivu, mtoto anyonyeshwe mara kwa mara na mama anatakiwa kufahamu ishara mbalimbali zinazoonesha kwamba mtoto ana njaa ambapo ishara.

No comments