Ads

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AFANYA ZIARA KUKAGUA VIWANDA VYA MBOLEA.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ameanza ziara ya siku 4 ya kutembelea Viwanda vinavyozalisha mbolea hapa nchini lengo likiwa ni kuona kiwango kinachozalishwa na viwanda vya hapa nchini na uwezo wake wa kuzalisha.

Akizungumza katika ziara hiyo leo iliyoanzia Jijini Dar es Salaam Katibu Kusanya amesema baada ya kupokea changamoto nyingi toka kwa wakulima kuwa wanauziwa mbolea kwa bei ya juu ameamua kufanya ziara ili ajue jinsi gani wanaweza kuwasaidia wenye viwanda ili wazalisha mbolea kwa wingi iwatosheleze wakulima.

"Mfano nilikuwa mkoani Kagera Mfuko wa kilo 50 wa mbolea ya Urea mkulima anaununua kwa shilingi elfu 80 hadi 90, nikagundua kuwa tatizo linalosababisha mbolea iuzwe kwa bei ghali ni kutokana na uchache wa viwanda ambavyo vinazalisha kwa kiwango kidogo ambacho hakitoshelezi mahitaji ya wakulima"Amesema Katibu Kusaya.

Aidha amesema takwimu zinaonyesha kuwa hapa nchini kuna viwanda 12 tu vinavyozalisha mbolea ambapo Minjingu ndio kiwanda pekee kikubwa kinachozalisha mbolea ambayo yapo chini ya mahitaji ya wakulima hapa nchini. 

Katika ziara hiyo aliofanya katika kiwanda cha Guavay Company limited kinachozalisha mbolea ya Organiki ya Hakika Katibu amesema mahitaji ya mbolea kwa Tanzania ni zaidi ya laki sita na nusu hivyo viwanda vilivyopo vikizalisha mbolea ni tani elfu 38 tu.

Katibu Kuyasa amesema upungufu huo wa mbolea unanababisha uagizwaji wa mbolea nyingi toka nje ya nchi hivyo kuwepp kwa changamoto kubwa ya uagizaji wa mbolea toka nje ya nchi 

Hata hivyo amesema serikali imeweka mikakati ya kuwashawishi wawekezaji kuwekeza katika viwanda vya mbole ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbolea hapa nchini na kupunguza changamoto ya bei kwa wakulima ili wazalishe kwa wingi.

Kwa upande wake Dkt Stephano Ngailo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRAC) amesema uzalishaji bado ni mdogo ukilinganisha na uhitaji ambapo kwa sasa uzalishaji ni asilimia 6 na mbolea toka nje ni asilimia 94.

Aidha amesema jitihada kubwa inafanywa na Serikali kuhakikisha kuwa uwekezaji mkubwa unafanyika katika viwanda vya mbolea ili kupunguza gharama za uwekezaji kwa mkulima ambapo lengo la mamlaka ya mbolea ni kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa mbolea bora kwa mkulima na kwa bei nafuu.

Naye Latifa Mafumbi mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Guavay Company limited amesema changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na udogo wa eneo la kuzalisha ambapo soko la mbolea za organiki linakuwa ambapo kwa mwaka wanazalisha tani elfu mbili huku uhitaji ukiwa ni tani elfu 20.

Hata hivyo ameiombo Serikali kuwasaidia kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa mbolea za Organiki kwani muamko wao ni mdogo sana ukizingatia mbolea hizo zinasaidia kurutubisha udongo kwani tafiti zinaonyesha kuwa udongo wa Tanzania rutuba yake inashuka.

No comments