Katibu mkuu Mifugo na Uvuvi ,ahimiza watanzania kufuga samaki
Aidha Wizara hiyo imesema kuwa kwasasa inatekeleza mradi wa matotolesho ya vifaranga vya samaki kupitia mradi wa usimamizi wa uvuvi wa kanda ya kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi (SwioFish), kwa lengo la kukidhi soko la mahitaji ya samaki nchini ili kuchochea uchumi wa viwanda.
Hayo yamebainisha na Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika viwanja vya maonesho ya ya 44 ya Biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 'Sabasaba'.
Amesema mkakati unaofanywa na serikali ni kwenye kuwekeza kwenye ufugaji wa samaki hivyo ni vyema wadau mbalimbali nao wakawekeza katika sekta hiyo.
Tamatamah amebainisha kuwa hapo awali tegemeo kubwa la samaki lilikuwa ni maji halisi lakini kwa sasa teknolojia za kisasa zimesaidia kupata samaki wengi kwa ajili ya mahitaji.
Hata hivyo amesema katika maonyesho ya mwaka huu watatumia kutoa changamoto kwa wavuvi kwa kutoa elimu ya kuvua samaki wanaofaa kuliwa.
"Wito wangu ni kwa wananchi au wadau wawekeze katika sekta ya uvuvi inalipa. Kwa miaka mitatu, miwili iliyopita kuna watu wamewekeza wanapata tani mbili au tatu kwa mwezi. Na mkakati unaoufanywa serikali ni kuwekeza kwenye ufugaji wa samaki, kwahiyo maonesho kama haya ni moja ya maeneo ya kuhamasisha wadau waweze kuwekeza katika sekta hii," amesema.
Akizungumzia kuhusu mradi huo, amesema mradi huo utasaidia kuibua sekta ya uvuvi na viwanda na kutoa fursa ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Amesema hivi sasa mradi huo unatekelezwa Kunduchi jijini Dar es Salaam ambao utagharimu dola za kimarekani ambapo ujenzi huo utaanza Oktoba mwaka huu.
"Mradi huu utasaidia kukuza sekta ya viwanda na uvuvi na kutoa elimu kwa wanafunzi ambao watapata fursaya kujifunza kwa vitendo,
tayari mchakato wa ujenzi wa maabara Kunduchi umeanza ambapo watashirikiana na chuo Kikuu na baada ya miezi mitatu ujenzi utaanza" Alisema
Post a Comment