Ads

TFNC YAHAMASISHA JAMII KUTUMIA CHUMVI YENYE MADINI JOTO .


Mwambawahabari

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania(TFNC) Dkt. Germana Leyna akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ,wakati wa ufunguzi wa semina ya waandishi wa habari kuhusu Udhibiti wa Tatizo la Upungufu wa Madini Joto Nchini.
Afisa Lishe Mtafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Anna John akizungumza na waandishi wa habari  juu ya Uthibiti wa Tatizo la Upungufu wa Madini Joto.
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyomba mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt.Germana Leyna wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wanahabari  juu ya Udhibiti wa Tatizo la Upungufu wa Madini Joto Nchini.
..................................................................................................................
Na Maria Kaira,Mwambawahabari
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetoa wito kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutumia Chumvi yenye Madini Joto toshelevu ili kuepuka madhara yatokanayo na  upungufu wa madini joto mwilini kwa lengo la kuikinga jamii kuwa salama .

Hayo yamesemwa na Afisa Lishe Mtafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Anna John wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye semina iliyohusu Udhibiti wa Tatizo la Upungufu wa Madini Joto Nchini Tanzania.

“Upungufu wa madini joto ni tatizo kubwa hapa nchini ni la tatu kwa ukubwa katika matatizo ya lishe ambapo huathiri makundi mbalimbali, pia tatizo hili linaathiri Afya na maendeleo ya jamii pamoja na uzalishaji mali na uchumi”amesema Anna.

Pia ameelezea athari zitokanazo na upungufu wa madini joto mwilini ni pamoja na kuharibika kwa mimba , udumavu, uvimbe wa tezi la shingo, kuzaa mtoto mwenye ulemavu pamoja na ulemavu wa akili na mwili.

Aidha Anna amesema jamii inatakiwa kuhifadhi chumvi yenye madini joto kwenye chombo safi chenye mfuniko na isikae karibu na moto au unyevunyevu kwa lengo la kuzuia upotevu wa madini hayo, ambapo amesema nchi imeamua kutumia chumvi kuchanganya na madini joto ili iweze kuwafikia watu wengi kwasababu asilimia kubwa ya watu wanatumia chumvi.

“Ukinunua chumvi yenye madini joto alfu bado unahifadhi wake sio mzuri bado haina maana hakikisha chumvi inaifadhiwa sehemu nzuri ili kuzuia upotevu wa madini joto, pia unaponunua chumvi hakikisha unasoma au unaangalia nembo ya mtoto anayecheka hapo utajua kama chumvi hiyo inamadini joto” amesema Anna.

Hatahivyo amewahamasisha wazalishaji wa chumvi hapa nchini kuhakikisha wanazalisha chumvi iliyochanganywa na madini joto kwa kiwango cha kiutaalam ili jamii ziwe salama na kuepuka kuathirika na ukosefu wa madini joto.

No comments