MKURUGENZI WA TAASISI YA KUMBILAMOTO FOUNDATION ATOA AHADI YA MSAADA KWA MTOTO MWENYE ULEMAVU.
Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya KUMBILAMOTO FOUNDATION Mhe. Omary Kumbilamoto kupitia Taasisi yake ya KUMBILAMOTO FOUNDATION ametembelea Shule Kontolengo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Vingunguti.
Katika ziara yake hiyo Mhe. Kumbilamoto alipokea ombe la viatu pamoja na Kiti Mwendo yaani Wheelchair kwaajili ya Mtoto mwenye ulemavu anayesoma katika Shule hiyo ya Kontolengo.
Taasisi ya KUMBILAMOTO FOUNDATION imejikita katika kusaidia Jamii ya watu wenye uhitaji, Kupitia Taasisi yake Mhe. Kumbilamoto amepokaea ombi hilo na kuwaahidi atawakabidhi kiti mwendo (Wheelchair) pamoja na viatua.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano Taasisi ya Kumbilamoto Foundation
Post a Comment