Makumbusho ya Taifa yazungumzi maadhimisho ya Miaka 61 ya siku ya Zinjanthroupus
MEELEZWA kuwa Wanaakiolojia waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus.
Ugunduzi huo ulifanyika Julai 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani.
Akizungumzia maadhimisho hayo kutoka Makumbuyo ya Taifa Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Dtk .Noel Lwoga alisema Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale alitoka Ulaya.
"Tanzania toka wakati huo wanasayansi na wanahistoria wanaamini kuwa asili ya mwanadamu ni bara la Afrika na eneo la Olduvai," alisema Dkt.Noel.
Alisema uwepo wa Zinjanthropus inathibitisha kuwa Tanzania ni chimbuko la watu duniani , makumbusho bado inatunza kumbukumbu hiyo baada ya Zinjanthropus kurudishwa nchi.
Aidha amewaomba watanzania kutembelea makumbusho ya taifa ili kujifunza katika kujua historia ya chimbuko la mwanadamu.
Kwa upande wake Dtk.Agness Gidna ambaye ni Mtafiti na Mhifadhi Mwandamizi Makumbusho ya Taifa alisema baada ya kupatikana fuvu hilo Tanzania historia ya tafiti ilianza Tanzania.
Kwa upande wake Dtk.Agness Gidna ambaye ni Mtafiti na Mhifadhi Mwandamizi Makumbusho ya Taifa alisema baada ya kupatikana fuvu hilo Tanzania historia ya tafiti ilianza Tanzania.
"Kugunduliwa kwa fuvu hilo kulifanya kugundulika kwa tabia za binadamu tangu miaka milioni mbili iliyopita ambapo mafuvu yameendelea kupatikana Afrika," alisema Dtk.Agness
Post a Comment