Ads

DC MSAFIRI KAAHIDI KUONGEZA UMEME KIWANDA CHA LAKE CEMENT

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri  akifurahi na wafanyakazi wa Kiwanda  Lake Cement baada ya zaezi la kuwazawadia wafanyakazi bora .

Na John  Luhende 
Mwamba wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri amewataka wafanyakazi wa kiwanda cha Lake Cement kinacho zalisha Cement ya Nyati  kufanya kazi kwa bidii kwani mchango wao ni mkubwa katika uzalishaji wa kiwandani hapo.

DC Msafiri ,ameyasemahayo alipotembelea kiwanda hicho katika hafla fupi ya kuwapongeza  wafanyakazi kiwandani hapo pamoja na kutoa zawadi mbalimbali kwa mfanya kazi bora  iliyoiliyofanyika kiwandani hapo ambapo amesema  kiwanda hicho kinatoa mchango mkubwa wa kodi  zaidi ya milioni 30.

"Ninyi mmekuwa wafanyakazi bora si kwa nguvu zenu peke yenu mmefika hapo kwa sababu kuna wenzenu waliwasidia ,unapoendesha taasisi  kubwa kama hii anapo patikana mfanyakazi bora huyo anakuwa amebeba tuzo yenu wote  taasi ili ifanikiwe haihitaji tu mtu mmoja nikama mchezo wa mpira unapasiwa mpira uanafunga goli kwahiyo msiwe wanyonge sana mkajisikia vibaya  fanyeni kazi kwa bidii na siku nyingine apate mwingine "Alisema

Alisema Kiwanda cha Nyati kimeajiri wafanyakazi zaidi ya elfu moja wakiwemo wafanyazi wa kudumu mianne  na kinazalisha zaidi  ya tani 6000  , kimechangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo ikiwemo mzunguko wa fedha katika maeneo hayo.

Cement ya Nyati ,  imekuwa ikitumika katika maeneo mbalimbali ya ujenzi wa miradi ya ya serikali ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa ,ujenzi wa mradi wa umeme Rufiji barabara na  madaraja .
Aidha DC Msafiri amesema  katika kuongeza ufanisi wa uzalishaji katika kiwanda hicho ameahidi kuongeza umeme  Megawhts 5.

"Najua kuwa mmeomba kuongezewa  umeme na mmepeleka maombi TPDC kuomba ges nataka niwathibitishie kuwa tutawalete  ,tunamradi mkubwa wa umeme eneo la Dege wenye thamani ya bilion 26 na unakamilika mwishoni mwa mwezi ujao  "Alisema

Pia alisema  Serikali  katika  Manispaa ya Kigamboni imepima  block 400 za viwanja kwajili ya viwanda na wamesha anza mchakato wa kufikisha ges katika maeneo hayo.

Pamoja na hayo ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwa wavumilivu katika kipindi kigumu cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19  kwani hawakufunga kiwanda na wala hawakupunguza wafanya kazi.

Hata hivyo DC Msafiri amewataka vijana  kuwa walinzi wa lasilimali za nchi na kukataa kushiriki katika vitendo vya kuvuruga amani kwani machafuko yakitokea yanarudisha nyuma maendeleo .

No comments