Bodi ya Michezo ya kubahatisha (GBT) yaipiga tafu TANTRADE vifaa vya kupambana na COVID 19 MAONESHO SABASABA.
Mwamba wa habari
Bodi ya michezo ya kubahatisha (GBT), imekabidhi msaada wa matanki 10 pamoja na sanitaiza kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade).
Mkabidhiano hayo yamefanyika leo katika viwanja vya maonesho ya ya biashara Sabasaba ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, James Mbalwe , ameeleza kuwa pamoja na majukumu ya kusimamia michezo yakubahatisha bodi hiyo pia inajukumu la kuhakikisha wanailinda jamii.
"Kwahiyo tukaona tushirikiane na Tantrade, kwa kuilinda jamii isiambukizwe na Corona kwasababu tunajua ugonjwa huu bado upo na unaua. Sisi tumeguswa sana tukaona tutumie fursa hii ya kusaidiana na wenzetu ili tuhusike kwa namna moja au nyingine kudhibiti ugonjwa huu.
"Ndio maana tumeleta vifaa vichache, havitaweza kukidhi mahitaji ya jamii inayokuja hapa lakini nafikiri tutaacha alama fulani ili watu wetu wasipate maambukizi. Kwahiyo nichukue fursa hii kuwaambia watanzania watembelee maonesho haya wasiwe na wasiwasi," amesema.
Aidha amesema pia wameanzisha, kampeni ya kumlinda mtoto kuhakikisha hashiriki michezo hiyo ya kubahatisha mpaka akiwa na umri chini ya miaka 18.
"Nichukue nafasi hii niwaombe watanzania waikumbatie kampeni yetu kwa kutokuwaruhusu watoto wadogo wasishiriki michezo hii.
"Tunajua ni burudani watoto wangependa kushiriki lakini wasubiri muda wao, utakavyofika wataweza kushiriki na kuburudika kama ilivyo kwa watu wazima," amesema.
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Naibu Mkurugenzi wa Tantrade, Latifa Khamis ameshukuru kwa msaada huo na kusema kuwa umekuja kwa wakati muafaka.
"Tunashukuru sana kwa msaada huu kwani umekuja wakati muafaka ambapo kuna tukio la kitaifa la maonesho ya sabasaba ambayo yamejumuisha wadau wote. Wametupatia vifaa ambavyo sisi tutaweza vitaweza kutusaidia katika kujikinga na maambukizi haya...kwahiyo tunawashukuru sana," amesema.
Post a Comment