Ads

YANGA YATAFUNA KIPOLO MWADUI BILA MORSON

Yanga Sports Club For Life - Naipenda yanga - Posts | Facebook

Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
Mabingwa wa kihistoria timu ya  Yanga SC wameng’ara ugenini baada ya kupata  ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga .

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Balama Elia Mapinduzi ‘Kipenseli’ aliyefunga bao hilo dakika ya sita tu ya mchezo akimalzia pasi ya Deus Kaseke baada ya shambulizi zuri lilioanzishwa na kiungo mwenzao, Haruna Niyinzoma ambalo liliokolewa na kipa wa Mwadui FC, Mahmoud Amir.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na Mbelgiji, Luc Eymael anayesaidiwa na mzawa Charles Boniface Mkwasa inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 28, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa wastani wa mabao tu na Azam FC, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wanaendelea kuongoza kwa pointi zao 71 za mechi 28 pia.
Mechi nyingine ya leo, wenyeji Coastal Union wamelazimishwa sare ya 2-2 na Namungo FC jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Issa Abushehe dakika ya 53 na Hance Masoud dakika ya 59 wakati ya Namungo yamefungwa na George Makang’a dakika ya tatu na Abeid Athumani dakika ya 17.

Ligi Kuu itaendelea kwa mechi mbili kesho, mabingwa watetezi, Simba SC wakiwakaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa na Azam FC wakiwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kikosi cha Mwadui FC kilikuwa; Mahmoud Amir, Yahya Mbegu, Khalfan Mbarouk, Joram Mgeveke, Augustino Simon, Enrick Nkhosi, Otu Joseph, Mussa Nampaka/ Mussa Chambega dk75, Raphael Aloba, Gerald Mathias/Abubakar Kambi dk82 na Omar Daga/ Wallace Kiango dk87.

Yanga SC; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed/Adeyum Salehe dk67, Lamine Moro, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Balama Mapinduzi/Abdulaziz Makame dk71, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi/David Molinga dk90+2, Patrick Sibomana/Yikpe Gilsaon dk62 na Deus Kaseke/Mrisho Ngassa dk85.

No comments