Ads

TANGA UWASA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI KUENDELEZA HUDUMA YA MAJI MARUNGU

Afisa
huduma kwa Wateja Tanga Uwasa ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkuu wa kitengo
cha Huduma kwa Wateja Rogers Machaku akizungumza wakati wa mkutano huo
kushoto anayemfuatilia kwa umakini ni 
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala

MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imesema
kwamba watatumia fedha za ndani kuendeleza mradi wa maji Marungu kadri
watakavyoweza ili mabomba yaweze kuwafikia wananchi kwa ukaribu ili
wanapoomba kuunganishiwa huduma hiyo iwe karibu kuliko ilivyo sasa.
Mradi
huo ulianza mwaka 2013 kwa ufadhili wa Serikali kupitia Programu
endelevu katika sekta ya maji ukisimamiwa na Halmashauri ya Jiji la
Tanga kabla ya Tanga Uwasa kukabidhiwa mwaka huu ili kuweza kuusimamia
mradi huo na kuuendeleza
Hayo yalisemwa na Mhandisi wa Ufundi wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
Mhandisi Rashid Shabani katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na
viongozi wa kata hiyo ambapo mamlaka hiyo ilipata nafasi ya kualikwa
kuhudhuria na kuweza kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya maji.
Alisema
baada ya kukabidhiwa mradi huo hivi sasa wanaangalia miundombinu
iliyokuwepo na mahitaji yaliyopo katika mji wa Marungu ili kuanza mara
moja shughuli za uendelezaji wa mradi huo ili kuweza kusogeza huduma ya
maji karibu na wananchi hatua itakayosaidia kuondosha kero hiyo.
“Mradi
huu baada ya kukabidhiwa sasa tumejipanga kutumia fedha za ndani kadri
tuwezavyo kuendeleza mradi huu na mabomba kuwafikia wananchi
kuwaunganishia maji kwa karibu kuliko ilivyo sasa hivi inaonekana bombo
limepita kwenye njia moja na ni kuu hivyo kwa mtu anayetaka maunganisho
nyumbani kwaka anaweza kuwa mbali hivyo tutaendeleza yaweze kupita
kwenye mita mbalimbali”Alisema
Hata hivyo Mhandisi huyo
aliwataka wananchi wanaoomba maji kuhakikisha barua zao zinapita kwenye
uongozi wa mtaa au kata ili kudhibitisha anapokaa ni kwake kwa sababu
wanaweza kuomba ukakuta kiwanja kina mgogoro na wao hawataki kuweka
miundombinu eneo lenye mgogoro kwa sababu hizo ni fedha za serikali na
ukiwekeza sehemu ambayo sio sahihi utapata hasara.
Mhandisi huyo
alisema tayari wataalamu wao wamekwisha kufika kwenye maeneo hayo
kuweza kuona vioski vya kuchotea maji vinasimamiwa na watu gani na hayo
maji wamepewa dhamana ya kuyasimamia na ikifika wakati wanaulizwa namna
walivyousimamia na kufikisha huduma kwa wananchi.
Awali
akizungumza katika mkutano huo Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed
Mambea aliishukuru Tanga Uwasa kwa kufika kwenye mkutano huo baada ya
kuwafuata ombi lake la kuwataka wataalamu wa mamlaka hiyo kuewaeleza
wananchi ni lini wanaweza kufanikiwa kufikishia maji majumbani mwao.
“Nishukuru
kwenye Kata yangu maji yamefika lakini hakuna mwananchi ambaye amwezea
kuunganishiwa maji nyumbani kwake nah ii imekuwa ni kero kubwa hivyo
tukaona tuwaalike kulizungumzia suala hilo ili liweza kupatiwa ufumbuzi
“Alisema

No comments